KIKOSI cha England kimewasili nchini England leo mchana kufuatia kuanza na ushindi wa 2-0 katika mechi za kufuzu Euro 2016 dhidi ya Uswisi.
Mchezaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck aliyefunga mabao tote hayo kwenye ushindi huo aliwasili akitabasamu, lakini mashabiki wa Gunners wanaweza kuwa walisononeshwa naye kumuona amebeba kibegi cha vifaa vidogo vidogo cha Manchester United.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amesajiliwa na Arsenal kwa Pauni Milioni 16 katika siku ya mwisho ya kufunga pazia la usajili kutoka Man United, lakini bado hajapatiwa begi la Arsenal.
Begi tatizo: Danny Welbeck (kushoto) akiwa ameshika kibegi cha vifaa vidogo vidogo cha Manchester United huku akitaniana na Phil Jones
Gunners: Hili ndilo begi la Arsenal analopaswa kubeba Welbeck kwa sasa
0 comments:
Post a Comment