Mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali
za Afrika mwakani nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe
iliyochezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh.
63,345,000.
Mapato hayo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa
Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 yametokana na washabiki 11,079
waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh.
10,000 na sh. 20,000.
0 comments:
Post a Comment