Tuesday 20 May 2014

NGORONGORO HEROES YAENDA NIGERIA

KIKOSI cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes chenye watu 25 kinaondoka kesho alfajiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).
Mechi hiyo itachezwa Jumamosi Mei 24 mwaka huu katika Jiji la Kaduna kwenye Jimbo la Kaduna ambalo lipo katikati ya Nigeria. Msafara wa timu hiyo unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi unaondoka kwa ndege ya Ethiopian Airlines. Ngorongoro Heroes inayonolewa na Kocha John Simkoko ilipoteza mechi ya kwanza iliyofanyika nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0.
Kikosi cha Ngorongoro kilichofungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza na Nigeria Dar es Salaam
Mwamuzi Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Atasaidiwa na Issa Yaya, Alfred Madjihoudel na Idriss Biani wote kutoka Tchad. Kamishna ni Aboubakar Alim Konate wa Cameroon.
 Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
 

0 comments: