Monday 19 May 2014

RASMI, VAN GAAL KOCHA MPYA MAN UNITED, GIGGS ASTAAFU KUCHEZA NA KUWA MSAIDIZI WAKE

HATIMAYE Manchester United imteua Louis van Gaal kuwa mocha wake mpya  baada ya kumfukuza David Moyes mwezi uliopita. 

Mholanzi huyo amesaini Mkataba wa miaka mitatu wa kazi Old Trafford, na atasaidiwa na Ryan Giggs - ambaye ametangaza kustaafu soka.
Frans Hoek na Marcel Bout wanajiunga na klabu hiyo kama makocha wengine wasaidizi, wakati Van Gaal - ambaye kwa sasa ni mocha wa Uholanzi anakuwa kocha wa kwanza wa kigeni katika klabu hiyo - ataanza kazi baada ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.

Mtaalamu wa Kihoanzi: Van Gaal ataanza kazi Man United baada ya kumaliza kuiongoza Uholanzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwezi ujao

Miezi 12 tangu Sir Alex Ferguson astaafu ukocha wa klabu hiyo, Van Gaal anaanzisha zama mpya katika mtindo mpya. 
"Yalikuwa matarajio yang wakati wore kufanya kazi katika Ligi Kuu ya England. Kufanya kazi kama mocha wa Manchester United, klabu kubwa duniani, inanifanya nijivunie sana,"alisema. 

WASIFU WA LOUIS VAN GAAL...

Louis van Gaal attends a press conference
Kuzaliwa: Agosti 8, 1951
Umri: Miaka 62
Alipozaliwa: Amsterdam, Uholanzi
Klabu alizochezea: Ajax, Royal Antwerp, Telstar, Sparta Rotterdam, AZ Alkmaar
Idadi ya mechi alizocheza: 333
Idadi ya mabao aliyofunga: 34
Klabu alizozifundisha: Ajax, Barcelona (two spells), AZ Alkmaar, Bayern Munich
Timu za taifa alizofundisha: Uholanzi (2000-02 na 2012-hadi sasa)
Mataji aliyoshinda akiwa kocha: Eredivisie (Ligi Kuu Uholanzi,1993-94, 1994-95, 1995-96, 2008-09), Kombe la UEFA 1991-92, Ligi ya Mabingwa Ulaya 1994-95, Super Cup ya UEFA (1995 and 1997), La Liga (Ligi Kuu Hispania,1997-98 na 1998-99), Copa del Rey (Kombe la Mfalme Hispania, 1997-98), Bundesliga (Ligi Kuu Ujerumani 2009-10

0 comments: