Monday 19 May 2014

JUMAMOSI MADRID KUHAMIA LISBON FAINALI REAL v ATLETICO!


>>NI ‘EL DERBI MADRILEÑO’ NDANI YA ESTÁDIO DA LUZ, LISBON, PORTUGAL!
 
UEFA CHAMPIONZ LIGI
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014
[Saa 3 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu]
Real Madrid v Atletico Madrid
Refa: Bjorn Kuipers [Holland] 
JUMAMOSI Mei 24, huko Lisbon, Ureno, UEFA CHAMPIONZ LIGI itaweka Historia mpya wakati Timu za Mji mmoja, Real Madrid CF na Club Atlético de Madrid, zikikutana kwenye Fainali ndani ya Estádio da Luz.
Hii ni Dabi ya Jiji la Madrid, El Derbi Madrileño, iliyohamia Lisbon, Ureno.
REAL_MADRID_PLAYERSHii ni mara ya kwanza katika Historia ya Miaka 59 ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa Timu za Mji mmoja kucheza Fainali hii.ATLETICO-DIEGO_COSTA_n_SIMEONE
PATA DONDOO NYINGINE MURUA:
-Fainali hii itakuwa ya 5 kwa Timu za Nchi moja kukutana.
-Wakati Real itakuwa ni mara ya 13 kucheza Fainali za Ulaya, Atletico wamewahi kucheza mara moya tu, 1973/74, walipotolewa na Bayern Munich baada ya kutoka 1-1 katika Mechi ya Kwanza na kupigwa 4-0 katika Marudiano Siku 2 baadae.
-Safari hii, Real Madrid wanawania kutwaa Taji lao la 10 la Ubingwa wa Ulaya walioubatiza ‘LA DECIMA’.
Mara pekee kukutana Ulaya
Timu hizi zimekutana mara 1 tu Ulaya Msimu wa 1958/9 kwenye Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na Real kushinda Bao 2-1 katika Mechi ya Kwanza na Atletico kushinda 1-0 katika Mechi ya Pili na ikalazimu ichezwe Mechi ya Tatu Siku 6 baadae na Real kushinda Bao 2-1 kwa Bao za Alfredo di Stéfano na Puskás huku Collar akiifungia Atletico.

El Derbi Madrileño:

-Jumla ya Mechi: 194
-Real Madrid: Ushindi 102
-Atletico Madrid: Ushindi 46
-Sare 46
Uso kwa Uso Msimu huu:
-Real na Atletico zimekutana mara 4.
-LA LIGA: Sept 28=Atletico 1 Real 0, Machi 2=Real 2 Atletico 2
-Copa del Rey: Feb 5=Real 3 Atletico 0, Feb11=Atletico 0 Real 2

0 comments: