Monday 19 May 2014

HOT NEWS; LUIS ENRIQUE KOCHA MPYA BARCELONA

KLABU ya Barcelona imemteua kiungo wake wa zamani, Luis Enrique kuwa kocha wake mpya.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 44, ambaye aliiongoza Celta Vigo msimu huu, amekubali Mkataba wa miaka miwili kurithi mikoba ya Gerardo Martino, ambaye ameachia ngazi baada ya msimu mmoja kazini.
Amepewa mikoba: Barcelona imemteua Luis Enrique, pichani. Hapa ni wakati alipokuwa kocha wa timu B
Klabu hiyo ya Katalunya imesema katika taarifa yake kwamba: "Bodi ya wakurugenzi ya FC Barcelona jioni hii imemthibitisha Luis Enrique Martineza kuwa kocha wao mpya wa kikosi cha kwanza, kufuatia mapendekezo ya Mkurugenzi wa Michezo, Andoni Zubizarreta. Luis Enrique, (Mwenye miaka 44), atasaini Mkataba wa miaka miwili,".
Barcelona pia imethibitisha kumuongezea Mkataba Leo Messi, kumsajili kipa Marc-Andre Ter Stegen kutoka Borussia Monchengladbach na kuwarejesha Rafa Alcantara na Gerard Deulofeu ambao walikuwa wakicheza kwa mkopo Celta Vigo na Everton.
Kuteuliwa kwa mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania ambaye alicheza Nou Camp kuanzia mwaka 1996 hadi 2004 alipojiunga nato akitokea wapinzani wa jade  Real Madrid, ni mwanzo mpya wa kurejesha heshima ya Barcelona iliyoshuka msimu huu.

0 comments: