Saturday 17 May 2014

HOT NEWS; KOCHA BARCA ABWAGA MANYANGA BAADA YA KUKOSA UBINGWA SIKU YA MWISHO

KOCHA Gerardo Martino amesema anaondoa Barcelona baada ya kumaliza msimu wake wa kwanza kazini vibaya akikosa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania katika sikh ya mwisho. 

Kocha huyo Muargentina amefikia makubaliano ya kuacha kazi baada ya Barcelona kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa wapya, Atletico Madrid usiku huu. 
Martino aliteuliwa kuifundisha Barca msimu huu ili kuendeleza wimbi la mafanikio Barcelona lililoanzishwa na Pep Guardiola mwaka 2008.  
Anaondoka: Gerardo Martino anaondoka Barcelona baada ya msimu mmoja tu kazini

Lakini Barcelona imemaliza msimu bila taji lolote kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2007-08. 
Mchezaji wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique anatarajiwa kuchukua nafasi ya Martino, ambaye anaondoka akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake. 
Enrique anaachia ngazi ukocha wa Celta Vigo baada ya kukutana na Barcelona wiki iliyopita.

0 comments: