Sunday 18 May 2014

, HOMA YA DENGUE YAHUSISHWA KWA KIFO CHA MSANII BONGO MUVI ADAM KWAMBIANA



Msanii maarufu wa filamu za maigizo hapa nchini, Adam Kuambiana amefariki Jana mida ya saa 5 asubuhi, huku kifo chake kikiambanata na hofu ya ugonjwa wa homa ya dengu unaotikisa nchi kwa sasa.

Kuambiana aliyekuwa akifahamika kwa kuwa mmoja wa wasanii wenye msimamo, alifariki dunia wakati akipelekwa Zahanati ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar.


Kabla alikutwa ameanguka chooni kwenye chumba alichopanga katika nyumba ya wageni ya Silver Rodge iliyopo Sinza Kwa Remmy jijini Dar.
 Mhasibu wa Silver Rodge ambaye alikataa kutaja jina lake alisema baada ya kumkimbiza msanii kwenye zahanati hiyo daktari alimpima na kuwaambia kuwa msanii huyo ameshaaga dunia.
Mwili wa msanii huyo umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya muhimbili.
MAREHEMU KUAMBIANA WAKATI WA UHAI WAKE (KATIKATI) HII NI FILAMU YA LOST SON, MOJA YA ZILE ALIZOIGIZA NA KUONYESHA UWEZO WAKE.

Hata hivyo, kumekuwa na hofu ya ugonjwa huo wa homa ya dengue kwa kuwa moja ya viungo vyake wazi vya mwili, vilikutwa vimetokwa na damu nyingi sana.
Huenda majibu ya mwisho ua uchunguzi wa mwili wake, yatatoa majibu sahihi kuhusiana na kifo cha msanii huyo.

KWA MASIKITIKO MAKUBWA, NAWAPA POLE FAMILIA YA MAREHEMU PAMOJA NA WASANII WA FILAMU NCHINI.
MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA.

0 comments: