Jeshi la Polisi nchini linadaiwa kumkamata Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Vijana wa Chama cha CUF, Katani Ahmed Katani jijini Dar es Salaam
kwa tuhuma za uchochezi na kumsafirisha kwa ndege kwenda mkoani Mtwara.
kwa msaada wananchi gazeti juni 1
Habari zilizolifikia Mwananchi Jumamosi na
kuthibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro zilieleza kuwa
Katani alikamatwa juzi mchana baada ya kupigiwa simu na maofisa wa
polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi jijini humo.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, Suleiman Kova alipoulizwa juu ya kukamatwa kwa kiongozi huyo
alisema hana taarifa huku akiomba apewe muda ili aulize.
“Sina taarifa ngoja niulize”, alisema kwa kifupi na hata alipotafutwa baadaye hakupokea simu yake ya mkononi.
“Alipigiwa simu juzi na maofisa wa polisi na
kuelezwa kuwa anahitajika kituoni hapo, lakini alipofika alikamatwa na
kuwekwa chini ya ulinzi” zilieleza habari hizo na kuongeza;
“Alihojiwa kwa saa kadhaa na jana asubuhi
alisafirishwa kwa ndege kupelekwa mkoani Mtwara. Walitaka kumsafirisha
kwa basi lakini viongozi wa CUF walikataa jambo hilo, hivyo kulazimika
kusafirishwa kwa ndege.”
Habari hizo zilifafanua kwamba kwamba sababu kubwa
ya kukamatwa kwa Katani ni kuhusishwa na vurugu zilizotokea mkoani
Mtwara kati ya wananchi wanaopinga mradi wa bomba la gesi kutoka mkoani
humo kwenda Dar es Salaam dhidi ya polisi.
Kwa upande wake Mtatiro alisema kuwa CUF hivi sasa
inajipanga kuweka mawakili kabambe kwa ajili ya kumtetea kiongozi huyo
wa vijana wa chama hicho.
“Tulijua tu kuna kiongozi wa chama atakamatwa
maana kwa muda mrefu Polisi wamekuwa wakisema kuwa watawakamata viongozi
wa juu wa chama. Kwa sasa Katani yupo Mtwara na sababu ya kukamatwa
kwake ni kutuhumiwa kuchochea vurugu za Mtwara” alisema Mtatiro.
kwa msaada wananchi gazeti juni 1
0 comments:
Post a Comment