SHIRIKA la ndege la Uturuki linawania kuchukua nafasi ya Samsung, ambao mkataba wao wa udhamini wa jezi za Chelsea unafikia tamati mwishoni mwa msimu.
Shirika hilo la ndege la nne kwa ukubwa Ulaya, ambalo liliingia mikataba ya kukumbukwa na nyota kama Lionel Messi na Kobe Bryant, hive karibuni limekuwa wadhamini wa Barcelona, Manchester United na timu ya taifa ya Uturuki.
Uzinduzi: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho (kushoto) na Mtendaji Mkuu, Peter Kenyon katika uzinduzi wa udhamini wa Sumsung mwaka 2005
Samsung imekuwa mdhamini wa Chelsea tangu mwaka 2005 wakati Mtendaji Mkuu wa zamani, Peter Kenyon aliposema klabu hiyo inakwenda kuipaka dunia rangi ya bluu.
Chelsea ilisaini tena Mkataba wake na Samsung mwaka 2013, lakini ajabu haikutangazwa sana.
Shirika la ndege la Uturuki limekuwa wadhamini wa Barcelona
Nyota: Shirika la nne la ndege kwa ukubwa Ulaya lilting Mkataba na Lionel Messi na Kobe Bryant
Shirika la Ndege la Uturuki pia lina uhusiano na Manchester United
Chelsea ilikubali Mkataba wa miaka 10 wa vifaa vya michezo wenye thamani ya Pauni Milioni 300 na adidas msimu uliopita.
Pamoja na hayo, kiwango kinaonyesha ni jinsi gani Chelsea iko nyuma ya Manchester United katika masuala ya kibiashara.
Mkataba wa timu ya Old Trafford wa vifaa vya michezo na Chevrolet, ambao klabu hiyo iliupata miaka miwili kabla ya kuanza kwake msimu wa 2014-15, una thamani ya Pauni Milioni 50 kwa msimu.
0 comments:
Post a Comment