Saturday 6 September 2014

RONALDINHO ASAINI MIAKA MIWILI MEXICO


KIUNGO wa zamani wa Brazil na Barcelona, Ronaldinho, mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka mara mbili, amesaini Mkataba wa miaka miwili na Queretaro, klabu ya Daraja la Kwanza Mexico. Klabu hiyo imesema jana.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye pia amechezea klabu za Paris St Germain na AC Milan, amekuwa mchezaji huru tangu Julai mwaka huu baada ya kuvunja mkataba wake na Atletico Mineiro ya Brazil.
"Tunayo furaha kubwa kuongeza ubora wetu wetu leo, mchezaji ambaye amefanya vizuri kwenye soka ya kimataifa. Bingwa wa dunia mwaka 2002, Mchezaji Bora wa Dunia 2004 na 2005, klabu imempa jina la utani Gallos (jogoo),"wamesema katika taarifa yao.

Jogoo: Ronaldinho amesaini Mkataba wa miaka miwili Queretaro ya Mexico

0 comments: