Saturday 6 September 2014

PIGO KWA CHELSEA; DIEGO COSTA AUMIA KUTEMWA KIKOSI CHA HISPANIA


MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa ameondolewa kwenye kikosi cha Hispania kitakachocheza mechi ya kuwania kufuzu kwenye fainali za Euro dhidi ya Macedonia kutokana na maumivu ya nyama za paka.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alisumbuliwa na matatizo kama hayo kwa miezi minne iliyopita na alilazimika kutolewa kwenye kikosi cha Hispania kilichofungwa 1-0 na Ufaransa katika mchezo wa kirafiki jana baada ya kuhisi maumivu.
Munir El Haddadi, mchezaji mwenye thamani kubwa wa Barcelona, ataziba pengo la Costa katika mchezo huo utakaofanyika Jumatatu mjini Valencia.
Majeruhi: Diego Costa ameondolewa kikosi cha Hispania baada ya kuumia nyama

0 comments: