Sunday, 7 September 2014

MECHI YA YANGA NA BIG BULLETS WAMALAWI YAYEYUKA GHAFRA JUA CHANZO NA SABABU YA KUTOKUCHEZA LEO



MCHEZO kati ya Yanga SC na Big Gullets ya Malawi uliokuwa ufanyike jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umefutwa kutokana na wageni kuharibikiwa na gari wakiwa njiani kuja nchini.
Mashabiki kadhaa wa wamefika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kushuhudia mchezo huo, lakini kwa bahati mbaya wakakuta hakuna hata dalili.
Taarifa zinasema Waandaaji wa mechi hiyo, Chama cha Soka Dar es Salaam  (DRFA) walifanya jiithada za kupata timu mbadala ya kucheza na Yanga, lakini zikashindikana.
DRFA walijaribu kufanya mazungumzo hadi na Gor Mahia ya Kenya iliyofungwa 3-0 na Simba SC jana, lakini pia imeshindikana.

MUDA HUO BIG BULLETS WA YANGA SC  WALIKUWA LIGI YA MALAWI LEO   NA WATOKA SARE 

KLABU ya Big Bullets iliyotangazwa kucheza mechi ya kirafiki na Yanga SC leo Dar es Salaam, jioni ya leo imetoka sare ya bila kufungana na Epac Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre katika Ligi Kuu ya TNM.
The Bullets sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa pointi zake 36 baada ya mechi 17, sawa na vinara Moyale Barracks ambao wanaongoza kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Katikati ya wiki, Yanga SC ilitangaza mchezo wa kirafiki na timu hiyo ya Malawi kwamba utafanyika leo na baadaye Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) kikasema, timu hiyo iliharibikiwa gari ikiwa njiani kuja Tanzania. 
Usanii gani huu? Big Bullets waliodaiwa kuharibikiwa gari wakiwa njiani kuja Dar es Salaam, wamecheza mechi leo Ligi ya Malawi na kutoka sare 0-0

MATOKEO LIGI KUU MALAWI WIKIENDI HII

Jana; Jumamosi:
Blue Eagles 4 Chikwawa United 1
Red Lions 1 Mafco 0
Blantyre 1 Epac 1
Azam Tigers 1 Mighty Wanderers 0
Leo; Jumapili:
Big Bullets 0 Epac 0
Kamuzu Barracks 0 Silver Strikers 2
Civo United 2 Chikwawa United 1
Airborne Rangers 3 Red Lions 0

0 comments: