LIGI KUU ENGLAND inarejea tena Jumamosi baada ya kupisha Mechi za Kimataifa kwa Wiki mbili na Mechi ya kwanza kabisa ipo Emirates na hii ni Bigi Mechi kati ya Arsenal na Manchester City ambao ndio Mabingwa Watetezi.
Mwezi uliopita, Arsenal iliichapa Man City Bao 3-0 Uwanjani Wembley kwenye Mechi ya kufungua pazia Msimu mpya kugombea Ngao ya Hisani lakini kwenye Ligi Arsenal wameshinda Mechi moja na kutoka Sare Mechi 2 zilizopita.
Nao Man City walianza kwa ushindi katika Mechi mbili za kwanza lakini kwenye Mechi yao ya mwisho Uwanjani kwao Etihad walitandikwa 1-0 na Stoke City.
Mbali ya Mechi hii, Chelsea, ambao wanaongoza Ligi kwa kushinda Mechi zao zote 3, watakuwa kwao Stamford Bridge kucheza na Swansea City ambao ndio wamefungana nao kileleni na ambao pia wameshinda Mechi zao zote 3.
Lakini Chelsea huenda wakamkosa Straika wao Diego Costa ambae ndie amewafungia Bao 4 katika Mechi 3 kwani Mchezaji huyo ana matatizo ya Mguu.
Baadhi ya Mechi nyingine 8 za Siku ya Jumamosi ni zile za Liverpool, bila Straika wao mkubwa Majeruhi Daniel Stirridge, kucheza na Aston Villa Uwanjani Anfield na Tottenham kucheza na Sunderland huku Everton wakiwa Ugenini kuivaa West Brom.
Jumapili ipo Mechi moja tu na Old Trafford itajaa shauku kubwa kwani Mashabiki wa Manchester United watataka kuona Wachezaji wao wapya 6 wakicheza pamoja kwa mara ya kwanza kuikabili QPR iliyopanda Msimu huu.
Mashabiki hao wanataka kujua Meneja Louis van Gaal kivipi atapangapanga Kikosi chenye wapya Marcos Rojo, Daley Blind, Anders Herrera, Luke Shaw, Angel Di Maria na Radamel Falcao kikishirikiana na Mastaa wa Klabu Wayne Rooney na Robin van Persie.
Jumatatu Usiku iko Mechi moja tu wakati West Ham United watakapocheza Ugenini na Hull City.
BPL-LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 13
1445 Arsenal v Man City
1700 Chelsea v Swansea
1700 Crystal Palace v Burnley
1700 Southampton v Newcastle
1700 Stoke v Leicester
1700 Sunderland v Tottenham
1700 West Brom v Everton
1930 Liverpool v Aston Villa
Jumapili Septemba 14
1800 Man United v QPR
Jumatatu Septemba 15
2200 Hull v West Ham
0 comments:
Post a Comment