Monday 1 September 2014

DALEY BLIND ATIA WINO MAN UNITED DK ZA MWISHONI

KLABU ya Manchester United imemsajili Daley Blind kwa dau la Pauni Milioni 14 katika jitihada za kocha Louis van Gaal kutatua tatizo la safu ya ulinzi Old Trafford.Hi imekuja dakika za mwishoni wakati usajili wa ligi kuu ulaya inaenda kufungwa leo saa 6 usiku
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uholanzi mara moja amwatumia salamu mashabiki wa timu hiyo kwa kusema; "Ni heshima kusajiliwa na United. Siwezi kusubiri kufanya kazi na klabu dunia,". 
Inamaanisha Van Gaal ametumia zaidi ya Pauni Milioni 150 kwa usajili wa kipindi hiki - ambacho ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutumiwa na klabu hiyo kwa miaka mitano iliyopita, huku Radamel Falcao naye akiwa mbioni kukamilisha uhamisho wa mkopo.

Tabasamu tupu:Manchester United imemsajili Daley Blind kwa Pauni Milioni 14 kutoka Ajax

0 comments: