Friday 5 September 2014

ANGALIA AJALI YA BASI ILIVYO UAWA MKOANI MARA MATUKIAO KATIKA PICHA


Habari za hivi punde zilizokifikia chumba cha habari cha mbeyagreennews blog ni kwamba kuna ajali mbaya imetokea katika eneo la sabasaba maarufu kama kwa wachina takribani kilomita 25 kutoka Musoma mjini mkoani Mara.
Inaelezwa kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu  na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 20 na majeruhi zaidi ya 70 katika eneo la Sabasaba wilayani Butiama.

Mbeyagreennews blog imeambiwa kuwa ajali hiyo imetokea wakati gari aina ya landcruiser kuingia barabarani ghafla ,ndipo Bas la Mwanza Coach  likitoka Musoma kwenda Mwanza likaivaa gari hiyo na wakati huo huo basi  la J4 Express likitoka Mwanza  kwenda Tarime nalo likagonga magari hayo.


Ajali hii imetokea majira ya saa 5 na nusu ,Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara

0 comments: