Sunday 18 May 2014

NSSF YAAHIDI NEEMA YA MAFAO KWA WACHEZAJI WA LIGI KUU TANZANIA

DSC_0081Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) umeahidi kuwa wachezaji wa timu za ligi kuu kuanzia mwakani watajiunga na mfuko huo ili kuweza kuwapa na kupata mafao mbalimbali ikiwemo mafao ya matibabu, ulemavu na mikopo ili waweze kunufaika na michezo yao kama ilivyo kwa nchi ambazo zimeeendelea duniani.

Akiongea na wadau wa mfuko huo mapema leo Jijini Arusha, , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Crinsetus Magori, alisema kuwa mpaka sasa tayari mfuko huo ulishaanza kufanya mazungumzo ba wadau mbalimbali wa michezo hapa nchini ili kuweza kuokoa maisha ya wachezaji
Magori alidai kuwa mpango huo utaanza rasmi mwakani na utaweza kuwanufaisha wachezaji mbalimbali hasa wale ambao wanachezea ligi kuu kama zilivyopangwa.

“tunataka kuona kuwa wachezaji wetu nao wanakuwa na mafao nah ii itaweza kuwajengea tabia ya kujiwekezea akiba kwa ajili ya maisha yao ya hapo baadae lakini kama wakiwa na mafao pia itasaidia kupata mahitaji ya muhimu hasa pale wanapokabiliwa na majanga kama ugonjwa pindi wanapokuwa uwanjani”aliongeza Magori
Magori alisema ni jambo la kusikitisha kuona au kusikia mchezaji akiumwa anakosa fedha ya kujitibia wakati kama angekuwa amejiunga na NSSF, angepata matibabu katika hospitali aliyeichagua bila malipo yoyote.

Magori, alisema kuwa NSSF, imeamua kuboresha huduma zake kwa kupanua wigo wa uandikishaji wanachama ikiwemo wachezaji wa ligi kuu ambao fedha zao zitakuwa zikikatwa moja kwa moja kutoka kwa wafadhili wa ligi hiyo.
“NSSF tumedhamiria kuboresha huduma zetu na kujitanua zaidi, wachezaji ni miongoni mwa walengwa wakuu baada ya kukamilisha kuwaandikisha wakulima na wachimbaji madini…tarajieni makubwa zaidi” alisema

Awali Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisema kuwa wachezaji hapa pamoja na wana sanaa mbalimbali katika Nchi ya Tanzania wanakuwa maarufu pindi wanapochezea timu mbalimbali lakini wanapoacha kucheza kutokana na sababu mbalimbali wanajikuta wakiwa wanaishi kwenye maisha magumu tofauti na majina yao kwenye jamii.
“Leo nimezungumza na Katibu Mkuu wa Simba, kaniambia kuanzia mwakani wachezaji wa timu hiyo wataingia katika mfumo wa kukatwa fedha zao na kuzipeleka NSSF ili wapate mafao saba yanayotolewa na mfuko huo, ningependa NSSF muangalie kundi hilo.

0 comments: