Monday 19 May 2014

ABDULRAHMAN KINANA ALA KWA MAMA NITILIE, AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI TABORA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Stendi ya zamani mjini Tabora wakati akihitimisha ziara yake ya siku 11 katika wilaya zote za mkoa huo, ikiwani na lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, Katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, kero  zilizochukua nafasi kubwa katika ziara hiyo ni Wizi wa fedha za malipo ya mauzo ya tumbaku kwa  wakulima wa mkoa huo, Suala la walimu wapya kutoingizwa katika utaratibu wa malipo ya mishahara yao ambalo limeshatatuliwa na walimu hao wameingizwa kwenye mfumo wa kompyuta na wataanza kulipwa mishahara yao mwezi huu lakini pia masuala ya ardhi na tatizo la maji, ambapo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana ameahidi kuwasilisha kero hizo kwa Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili zifanyiwe kazi kupata ufumbuzi wa kudumu.(
1a 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mlo wa mchana kwa mama Nitilie katika stendi mpya ya mabasi mjini Tabora kushoto ni Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Mh. Aden Rage na Katikati ni Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Tabora Mh. Munde Tambwe wakishiriki pamoja naye katika mlo huo. 2 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwashukuru wazee wa kabila la Wanyamwezi mara baada ya kumsimika kuwa chifu wa kabila hilo mkoani Tabora 2a 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mlo wa mchana kwa mama Nitilie katika stendi mpya ya mabasi mjini Tabora kushoto ni Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Mh. Aden Rage na Katikati ni Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Tabora Mh. Munde Tambwe wakishiriki pamoja naye katika mlo huo pamoja na vijana wa mjini Tabora 3 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo na Mh. Samwel Sitta Mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki mara baada ya kusimikwa rasmi kuwa chifu wa kabila la wanyamwezi mkoani Tabora leo. 4 
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa mjini Tabora katika mkutano wa hadhara uliofanyika stendi ya zamani. 5 
Stephen  Wassira Mbunge wa jimbo la Bunda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) akiwahutubia wananchi wa Tabora mjini. 7 
Mbunge wa jimbo la Sikonge mkoani Tabora Mh. Said Mkumba akihutubia katika kutano huo. 8 
Wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano huo. 9 
Wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano huo. 10 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu akizungumza katika mkutano huo. 11 
Mh. Livingstone Lusinde mbunge wa jimbo la Mtera akizungumza na wana Tabora. 12 
Stephen  Wassira Mbunge wa jimbo la Bunda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) kulia, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo Mh. Samwel Sitta katikati na Mbunge wa jimbo la Tabora Mh. Aden Rage wakiwa katika mkutano huo. 13 
Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya akipata mlo wa mchana kwa mama nitilie leo mchana katika stendi kuu ya mabasi mjini Tabora wakati Katibu wa mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipoongoza msafara wake kwenda kula hapo. 14 
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwassa nao wakipata mlo wa mchana kwa  mama Nitilie stendi kuu ya mabasi mjini Tabora.  15 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye  kushoto na Mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwassa wakielekea stendi kuu ya mabasi ya mjini Tabora wakati wakienda kupata mlo wa mchana kwa mama Nitilie

0 comments: