Wednesday 6 August 2014

Waadhibiwa kwa kukejeli wajakazi Afrika kusini

 

Wanafunzi hawa walidhibiwa kwa kosa la kukejeli waafnyakazi wa nyumbani
Chuo kikuu cha PRETORIA kimechukua hatua za kinidhamu dhidi ya Wanafunzi wa kike baada ya kuonekana kwenyePICHA wakiwa wamevaa mavazi yanayowaonyesha kama wafanyakazi wa nyumbani .
Kwa mujibu wa mtandao wa EYE WITNESS NEWS , shuhuda wa picha hizo aliripoti kwa uongozi baada ya kuona picha hizo kwenye ukurasa waFACEBOOK, baadae picha hizo zikafutwa.
Wakiwa na nyuso zilizopakwa rangi YA kahawia huku wakiwa wamefungasha mito kwenye makalio yaonekane makubwa, kisha wakapiga picha.
Walivalia mavazi ambayo huaminika kuvaliwa na wafanyakazi wa majumbani huku wakitabasamu hali iliyoashiria kuwa mzaha.
Uongozi wa chuo unasema pamoja na kuwa picha hizo zilipigwa katika mazingira ya sherehe binafsi, hali ya kuwa ni wanafunzi wa chuo hicho hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa kosa la kutia dosari jina la chuo.
Mkuu wa chuo hicho Nicole Mulder amesema chuo hakitavumilia vitendo vyenye kuashiria ubaguzi wa rangi.
Wanafunzi hao hawajajibu tuhuma zozote dhidi yao, pia tume ya haki za binaadamu nchini AFRIKA KUSINI imesema haijapokea malalamiko yoyote kuhusu picha hizo.

0 comments: