Wednesday 6 August 2014

LIVERPOOL YASAJILI BONGE LA BEKI KUTOKA ATLETICO MADRID

 

KLABU ya Liverpool imetangaza kumsajili beki wa kulia wa Atletico Madrid, Javier Manquillo kwa mkopo.
Beki huyo wa kulia atakwenda kugombea namba na GLEN JOHNSON katika jitihada za kocha Brendan Rodgers kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya.
Manquillo, ambaye ana umri wa miaka 20 tu, alitemwa na REAL MADRID akiwa na umri wa miaka 14 tu, lakini tangu hapo amezichezea timu zote za taifa za vijana za Hispania kuanzia chini ya umri wa miaka 16 hadi miaka 20. 

Mpiganaji mpya: Liverpool imetangaza kumsajili beki wa kulia wa Atletico Madrid, Javier Manquillo kwa mkopo

0 comments: