Saturday 9 August 2014

Hii ndiyo nyumba ya Mch. Rwakatare iliyovunjwa yenye thamani mamilioni


Rungu la Sheria limetua kwa Mch.Gertrude Rwakatare,Mchungaji Kiongozi wa 'Mlima wa Moto'.Ni nyumba yake iliyokuwa Mbezi Beach. Alijenga katika eneo la mjane alilolivamia. Hatimaye sheria imechukua mkondo wake. Mjane alilia kwa furaha. Nyumba hiyo ilisajiliwa kwa jina la mtoto wa Mch.Rwakatare. Uboboaji huo ulifanywa chini ya ulinzi mkali wa askari waliokuwa wamesheheni silaha za moto.

Wakati wa ubomoaji,alijitokeza mtu mmoja aliyedai kuwa ni Wakili wa mwenye nyumba akiwa na nyaraka za kimahakama zinazodaiwa kuweka zuio la kubobolewa kwa nyumba hiyo.Hatahivyo,alipuuzwa na ubomoaji kuendelea kama ulivyopangwa. Kweli sheria ni msumeno!

Chanzo: ITV
Serikali yabomoa nyumba za mamilioni Mbezi Beach 

Katapila likibomoa moja ya nyumba nne za Tibe John katika eneo la Mbezi Beach, Dar esSalaam jana.
Picha na Beatrice Moses. 

Na Beatrice Moses na Ally Nguba, Mwananchi

Kwa ufupi
Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314 chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.
Dar es Salaam.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imebomoa nyumba nne zenye thamani ya Sh800 milioni mali ya Tibe K. John zilizojengwa katika eneo la Mbezi Beach bila kibali na kinyume na sheria za mipango miji.


Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314 chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.

Wakati wa ubomoaji huo uliosimamiwa na Manispaa ya Kinondoni chini ya Mhandisi Baraka Mkuya, kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi wenye bunduki na mabomu ya machozi, wakiongozwa na Ofisa wa Operesheni, Emmanuel Tille.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Alphayo Kidata alisema kuwa ametoa agizo hilo kwa sababu sheria zinapaswa kuzingatiwa na kwamba nyumba hizo zilijengwa bila kuwa na kibali chochote cha manispaa kama inavyotakiwa.

“Kuwapo kwa kesi mahakamani hakuzuii sheria nyingine kutekelezwa, wamejenga hawana kibali,” alisema Kidata.

Wakili wa John, Emmanuel Augustino alidai kwamba hatua hiyo imetekelezwa kibabe na katibu mkuu, kwa kuwa kuna kesi wamefungua katika Baraza la Ardhi Kinondoni ambayo inaendelea kusikilizwa.
“Anajua wazi kuwa alichokifanya ni kinyume cha sheria, ameingilia uhuru wa mahakama,” alisema.

Augustino alisema hawajui watamshtaki nani ili kudai fidia, hasa kwa kuwa katibu mkuu alitoa agizo la mdomo na hakuna barua yoyote aliyoandika ambayo ingeweza kutumika kama ushahidi.
Wakili wa anayedaiwa kuwa mmiliki wa kiwanja hicho cha Janet Kiwia, ambaye ni HowardMsechu kutoka katika Kampuni ya Uwakili ya Homac, alisema wamefurahishwa na hatua hiyo kwa sababu walikiuka amri ya Baraza la Ardhi ya kupiga marufuku shughuli za ujenzi kuendelea.
CHANZO: Mwananchi
Last edited by Petro E. Mselewa; 7th August 2014 at 22:11.

0 comments: