Sunday, 18 May 2014

MAN CITY YAADHIBIWA NA UEFA KWA KUKIUKA FFP!


MAN_CITY-BINGWA_COC2014MANCHESTER CITY imepewa Adhabu na UEFA kwa kukiuka Sheria za FFP [Financial Fair Play] ambazo zinataka Klabu zijiendeshe kwa Mapato yao wenyewe kwa kupigwa Faini ya Pauni Milioni 49 na Kikosi chao kubanwa kisizidi Wachezaji 21 na 8 kati yao ni lazima wawe Wachezaji Chipukizi waliokuzwa Nyumbani kwenye Mechi zao za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Pamoja na hayo pia wametakiwa Msimu ujao wasizidishe Fungu la Fedha za Mishahara ya Wachezaji wao kupita lilivyo hivi sasa.
Kwenye Faini, City wametakiwa walipe Pauni Milioni 18 tu na nyingine kusimamishwa kuangaliwa mwenendo wao.
Mara baada ya kutangazwa Adhabu hiyo, Man City wamemesema wao hawakubaliani na uamuzi huo kwani wanaamini hawakukiuka FFP na hivyo watalipeleka mbele suala hili.
Vile vile, City wamesema kwenye Msimu huu wa UEFA CHAMPIONZ wao walitumia Wachezaji 21 tu hivyo hiyo Adhabu ya kuwabana wasizidishe Wachezaji 21 haitawaathiri sana.
Inaaminika Adhabu hiyo ni sawa na ile waliyopewa Paris Saint Germain kwa pia kukiuka FFP kama zilivyotolewa na Bodi ya Udhibiti Fedha ya UEFA, CFCB, [Club Financial Control Board].
Chini ya Sheria za FFP, Klabu zinatakiwa zisipate Hasara ya zaidi ya Pauni Milioni 37 katika Misimu miwili iliyopita.
Man City wao wamepata Hasara inayokaribia Milioni 149 kwa Misimu miwili iliyopita ikiwa ni Pauni Milioni 97 Mwaka 2012 na Pauni Milioni 51.6 kwa Mwaka 2013.
Man City na PSG ni miongoni mwa Klabu 9 ambazo zimetinga kwa CFCB na kupewa hadi mwishoni mwa Wiki hii kufikia makubaliano na UEFA  kuhusu Adhabu zao.
City wakikata Rufaa watasikilizwa na Jopo Maalum ambalo uamuzi wake hauna mjadala na upo uwezekano wa kuamuliwa Kifungo kwa City kutocheza Ulaya.

0 comments: