Kocha wa Ghana Kwesi Appiah amewaita kwenye Kikosi chake cha kuikabili Egypt hapo Oktoba 15 huko Kumasi ambapo Mshindi ndieanapewa
Tiketi ya kwenda Brazil Mwakani kucheza Fainali za Kombe la Dunia,
Wakongwe Sulley Muntari na Kipa Richard Kingson kwenye Kikosi cha
Wachezaji 25.
Muntari, mwenye Miaka 29 na anachezea AC
Milan huko Italy, aliachwa kwenye Kikosi cha Ghana cha Mwezi Septemba
kilichoibwaga Zambia na kufuzu kucheza Raundi ya Mwisho ya Mtoano dhidi
ya Egypt.
+++++++++++++++++++++++++
KOMBE LA DUNIA 2014 AFRIKA
Raundi ya Mwisho ya Mtoano
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Mechi za Kwanza:
Jumamosi Oktoba 12
19:00 Burkina Faso v Algeria
20:00 Ivory Coast v Senegal
Jumapili Oktoba 13
16:00 Ethiopia v Nigeria
20:00 Tunisia v Cameroon
Jumanne Oktoba 15
19:00 Ghana v Egypt
Marudiano:
Jumamosi Novemba 16
18:00 Nigeria v Ethiopia
22:00 Senegal v Ivory Coast
Jumapili Novemba 17
17:30 Cameroon v Tunisia
Jumanne Novemba 19
19:00 Egypt v Ghana
21:15 Algeria v Burkina Faso
**FAHAMU: Washindi 5 ndio watacheza Fainali za Kombe la Dunia
+++++++++++++++++++++++++
Kipa Richard Kingson, Miaka 35,
hajaichezea Ghana kwa Miaka miwili sasa na mara ya mwisho aliichezea
Blackpool ilipokuwa Ligi Kuu England Mwaka 2011 na tangu wakati huo
hajaitwa kuichezea Ghana lakini sasa amejiunga na Klabu ya Cyprus Doxa
Katokopia na ndio sababu iliyomfanya aitwe tena.
Pia Kocha amewaita tena kwenye Kikosi chake Jordan Ayew na Akaminko.
Bada ya Mechi ya huko Kumasi hapo Oktoba
15, Ghana na Egypt zitarudiana Mjini Cairo Novemba 19 na Mshindi kwenda
Brazil ikiwa ni moja ya Timu 5 zitakazotoka Afrika kucheza Fainali za
Kombe la Dunia.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Fatau Dauda (Orlando Pirates), Richard Kingson (Doxa Katokopias), Adam Kwarasey (Stromgodset)
MABEKI: David Addy
(Vitoria Guimaraes), Jerry Akaminko (Eskisehirspor), Mohammed Awal
(Maritzburg United), John Boye (Stade Rennes), Samuel Inkoom (Dnipro
Dnipropetrovsk), Daniel Opare (Standard Liege), Baba Abdul Rahman
(Greuther Furth), Rashid Sumaila (Mamelodi Sundowns)
VIUNGO: Albert Adomah
(Middlesbrough), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese), Kwadwo Asamoah
(Juventus), Christian Atsu (Vitesse Arnhem), Andre Ayew (Olympique
Marseille), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Michael Essien (Chelsea),
Emmanuel Frimpong (Arsenal), Sulley Muntari (AC Milan), Mubarak Wakaso
(Rubin Kazan)
MAFOWADI: Jordan Ayew (Olympique Marseille), Asamoah Gyan (Al Ain), Mahatma Otoo (Sogndal), Abdul Majeed Waris (Spartak Moscow)
Wednesday, 02 October 2013 10:14
0 comments:
Post a Comment