Viongozi wawili wa kundi la wabaguzi wa Afrika Kusini lililojulikana
naka "Boer Army" lililokula njama ya kumuua Rais wa Kwanza wa asili ya
Afrika, Nelson Mandela na kisha kuwafuta kabisa watu weusi nchini humo,
wamehukumiwa vifungo vya miaka 35 jela kila mmoja na mahakama kuu ya
Pretoria nchini humo.
Shirika la habari la Afrika Kusini, SABC limesema hukumu hiyo imetolewa leo baada ya kuendeshwa kwa miaka 10.
Mahakama
iliyotoa hukumu hiyo ilimkuta kiongozi Mike du Toit, aliyekuwa Mhadhiri
wa Chuo Kikuu na hatia katika kosa hilo wakati yeye akiongoza
mipango ya kuipindua Serikali mwaka 2002 kwa madhumuni ya kukiangusha na
kukifutilia mbali kabisa chama cha ukombozi cha ANC.
Viongozi wengine takriban 20 walihukumiwa vifungo vya chini ya miaka 35.
Tuesday, 29 October 2013
HOME »
» KABURU ALIYEPANGA KUMWUA MANDELA AHUKUMIWA MIAKA 35 JELA
0 comments:
Post a Comment