Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na wafanyakazi wa Swissport katika uwanja wa ndege wa
kimataifa ya Julius Nyerere wakati akielekea kwenye ndege jioni ya jana,
Jumatatu, Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya
kikazi ya siku nne ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali
Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu wa
Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe na Meneja wa Shirika
la ndege la Emirates uwanjani hapo Bw. Aboubakar Jumaa. (picha: Ikulu)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatatu, Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa

Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun.
Mkutano huo wa siku mbili utafanyika keshokutwa Jumatano na Alhamisi kwenye Ukumbi wa Queen Elizabeth 2 mjini London.
Miongoni mwa mambo makuu ambayo mkutano huo utazungumzia ni Serikali Uwazi na Ajenda ya Maendeleo Baada ya Mwaka 2015 wakati muongo wa utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millenium Development Goals) unafikia mwisho.
Masuala mengine ambayo yatazungumzwa katika mkutano ambao Rais Kikwete anaambatana na Mawaziri wake watatu ni pamoja na uwazi katika manunuzi ya umma, uwazi katika mikataba, haki ya kupata habari, uwazi katika ukaguzi wa fedha za umma, uwazi wa Serikali na vyombo vya habari, uwazi katika mikataba ya maliasili, uwazi katika maendeleo ya nchi zinazoendelea.
Mawaziri wanaoambatana na Rais Kikwete katika ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe, Waziri wa Sheria na Katiba Mheshimiwa Mathias Chikawe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar Mheshimiwa Mwinyihaji Makame.
Rais Kikwete anatarajia kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 2, 2013.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

0 comments:
Post a Comment