Wednesday, 30 October 2013

MTOTO ALIYEBAKWA NA BABA YAKE AOMBA ASAIDIWE APATE HAKI YAKE

Mtoto aliyefanyiwa ukatili kwa kubakwa na kulawitiwa na baba yake mzazi huko kijijini Kiria katika kata ya Mamba Kusini wilaya ya Moshi Vijijini ameomba msaada wa wanaharakati, wanasheria na taasisi huska ili apatiwe haki yake.

Mtoto huyo ambaye kwa sasa analelewa na msamaria mwema, amesema kamwe hatakaa asahau mateso aliyoyapata na 
angependa kuona baba yake akipewa hukumu inayostahili kwa maovu alioyoyatenda kiasi cha kusababisha mdogo wake kutoroka na hadi sasa haifahamiki alikotokomea.

Baba mzazi wa mabinti hao wawili aliripotiwa kuwabaka na kuwalawiti binti zake hao wenye umri wa miaka 10 na 13 na kuwajeruhi vibaya.

Wakinamama wa kijiji hicho walipopata taarifa hizo walishikwa na hasira, wakamkamata mtuhumiwa na kumpeleka kwenye Kituo cha Polisi Himo na wakatishia kumtoa uhai endapo polisi watamwachia huru, kwa madai imekuwa ni kawaida yao kila akifikishwa kituoni hapo kuhusiana na unyama anaowafanyia watoto hao huachiwa.

Imedaiwa mzazi huyo alianza kuwatenda wanawe unyama huo baada ya kuachana na mkewe kutokana na ugomvi baina yao na kwa kuwa aliachiwa watoto, ndipo alipoanza kuwatumia wote kwa zamu na kuwatisha kuwa endapo wangesema kokote kuhusu wanavyofanyiwa, angewaua.

Taarifa iliyotolewa na daktari wa Hospitali Teule ya Kilema baada ya kumpima mtoto huyo, ilionyesha kuwa aliharibiwa sehemu zote mbili za kutolea haja na kuota vijinyama ambavyo kwa sasa amepatiwa dawa ya kutumia kwa muda wa siku 14 na endapo havitaisha, atalazimika kufanyiwa upasuaji.

 
Source: /www.wavuti.com.bofya hapa kusikiliza sauti ya habari hiyo

0 comments: