Thursday, 17 October 2013

BAKWATA YA MALIZA MGOGORO NA VIONGOZI WA WILAYA YA ARUMERU

Picture
Kushoto ni Mjumbe wa baraza la mashehe wilaya ya Arumeru, Haruna Hussein Lotta, pembeni ni viongozi wa zamani wakikabidhiana rasmi ofisi (picha: JamiiBlog)
BARAZA kuu  la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetatua mgogoro uliokuwepo kati  yao na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Arumeru na Katibu  wa Wilaya wa baraza hilo baada ya kusimamishwa nafasi zao za uongozi kwa miezi  saba.

Kaimu katibu  wa (BAKWATA) mkoa wa Arusha, Abdallah Masoud alisema kuwa bazara  hilo limefikia hatua ya kuwarudisha
viongozi hao kwenye nafasi zao baada ya kusimamishwa katika nafasi hizo kutokana na  ukwiukaji wa sheria walioufanya wakiwa madarakani kinyume cha sheria cha baraza hilo.

Alisema kuwa, baada ya baraza kuu kukaa na kufanya  vikao vyake, walipitia barua mbalimbali zilizoandikwa na viongozi hao za kuomba kurudi katika nafasi  hizo huku wakikiri kutorudia tena makosa waliyofanya ndipo baraza hilo lilipopitia na kuwarudisha tena katika  nafasi.

‘Sisi dini yetu inaturuhusu kusamehe na kuwasikiliza watu mbalimbali katika shida zao ikiwemo kutatua migogoro mbalimbali iliyopo katika misikiti yetu lengo likiwa ni kuhakikisha kila mmoja wetu anaishi kwa amani  na kuondoa tofauti miongoni mwa waumini wetu kwani ndio lengo letu la kuleta amani kwa waumini na viongozi wetu kwa ujumla’ alisema Kaimu katibu huyo.

0 comments: