Wakili Mabere Marando, amedai Mahakama
ya Rufani, iliteleza kisheria katika uamuzi wake ambao uliwatia hatiani
na kuwahukumu kifungo cha maisha mwanamuziki Nguza Vikings au 'Babu
Seya' na mwanawe Johnson Nguza 'Papii Kocha'.
Marando alidai jana mbele ya jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani lililotoa hukumu hiyo, likiongozwa na Jaji Natharia Kimaro, kwamba mahakama iliteleza kwa kutozingatia miongozo ya kisheria ya nanma ya kuchukua ushahidi wa

mtoto, kutoitwa kwa mashahidi muhimu. Mbali na Jaji Nathalia, Majaji wengine ni Mbarouk Mbarouk na Salum Massati.
Wakili huyo, alidai hayo wakati wa kusikilizwa kwa maombi ya mapitio ya hukumu hiyo, iliyotolewa Februari, 2010, Jopo hilo liliwatia hatiani Babu Seya na mwanawe Papii na kuwapa adhabu ya kifungo cha maisha. Jopo hilo liliwaachia huru watoto wengine wa Babu Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza.
Marando alidai mahakama hiyo ilijiridhisha kulikuwa na makosa katika kupokea ushahidi wa watoto na kwa sababu matakwa ya sheria hayakufuatwa hivyo ushahidi huo ulipaswa kufutwa na waleta maombi kuachiwa.
"Mlikubaliana na sisi kwamba Mahakama ya Kisutu ilikosea haikuzingatia uchukuaji wa ushahidi lakini mlisema ilimradi kuwe na ushahidi wa kuunga mkono. Sisi tulisema hapana,"alidai.
Pia, alidai mahakama hiyo, ilikosea katika hukumu yake kwa kusema kuna shahidi wa 13 aliyedai kwenye nyumba ya Babu Seya kuna mlango wa siri ambao mtu anaweza kuingia na asionekane, ushahidi ambayo haupo na wala shahidi huyo hakusema hivyo.
“Mashahidi walisema wao waliona katika nyumba ya Babu Seya kuna milango miwili wa mbele na nyuma na yote inainghia sebuleni, mtu huwezi kuingia katika chumba chochote bila kupitia sebuleni... Sasa katika ukurasa wa 38 wa hukumu yenu, mmetamka kwamba shahidi wa 13 aliiambia mahakama kuna mlango fulani wa kuingia katika nyumba bila ya mtu mwingine kukuona. Ushahidi huo haupo katika ushahidi wa shahidi wa 13 hawakusema. Haya ndiyo mambo yanayojidhihirisha kuna kuteleza," alidai Marando.
Aidha, alidai katika ushahidi wa mashahidi wanaohusika na ushahidi uliowatia hatiani Babu Seya na Papii Kocha, walidai walikuwa wakiingia katika nyumba hiyo wakitokea dukani kwa Mangi ambaye alikuwa akijua kinachotokea.
Marando alidai kwa mujibu wa sheria, upande wa Jamhuri ulipaswa kumleta Mangi ambaye ni shahidi muhimu ili aje kuthibitisha, lakini katika hukumu yao walisema upande huo una hiari wa kumuita shahidi wanayemtaka, kauli ambayo ni kinyume cha sheria.
Alidai kuna kijana anaitwa Size ambaye anadaiwa alikuwa anawakusanya watoto wa kike na kuwapeleka kwa Babu Seya na kufanya kinachodaiwa kutendeka, lakini hakuitwa na wala mahakama hiyo katika hukumu haye haimkumzungumzia.
Hoja nyingine, Marando anadai mahakama hiyo, iliteleza kwa kutotoa maoni yake juu ya utetezi wao, kuhusu uwepo wa watu katika nyumba ya Babu Seya, ambao walidai ingekuwa si rahisi watoto kuingia bila ya wao kuwaona kwa kuwa kuna milango miwili ambayo inaingia sebuleni.
"Naomba mpitie tena hukumu yenu na kurekebisha mambo ninayoona yana makosa ya kiuterezi na mkikubaliana nasi mfute washitakiwa kutiwa hatiani na mfute adhabu zao," aliomba Marando.
Upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Jackson Bulashi, akishirikiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Mwangaza Mwipopo, Emmaculata Banzi, Joseph Pande na Wakili wa Serikali Apimaki Mabrouk.
Wakili Bulashi aliiomba mahakama hiyo, kutupilia mbali maombi hayo kwa sababu yalishatolewa uamuzi katika rufani waliyokata waleta maombi. Alidai kwa upande wao wanaona hakuna makosa yaliyofanywa katika kufikia uamuzi huo na kwamba kilichowasilishwa ni sababu za rufani ambazo tayari zilishatolewa uamuzi.
Jopo la Majaji lilisema kuwa limesikia hoja za pande zote na kwamba wataarifiwa tarehe ya kutolewa uamuzi. Awali, jopo hilo lilitupilia mbali maombi ya mapitio yaliyokuwa yamewasilishwa na Babu Seya na Papii Kocha mwenyewe kwa msaada kutoka gerezani, kwa kuwa hawakutumia vifungu sahihi kuyawasilisha.

Na
FURAHA OMARY, gazeti la Uhuru —
MWANAMUKIZI wa muziki wa dansi nchini Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae Johnson Nguza 'Papi Kocha Mtoto wa Mfalme', wameiomba Mahakama ya Rufaa nchini iifanyie upya hukumu yake iliyoitoa Februali mwaka 2010 ambayo iliwahukumu kifungo cha maisha kwasababu hukumu hiyo ina utetelezi wa wazi wa kisheria.
Ombi hilo Na.5/2010 liliwasilishwa kwa niaba yao na wakili wao Mabere Marando jana mbele ya jopo lilelile lilotoa hukumu ya awali ya Februali 2010 ambalo linaongozwa na Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk .S.Mbarouk.
Wakili Marando alidai kwa mujibu wa kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 inatoa mamlaka kwa mahakama ya rufaa kufanya mapitio ya hukumu inazozitoa hivyo wateja wake wamewasilisha ombi hilo la mapitio kwasababu wanaamini mahakama yake ilikosea wazi wazi kisheria katika hukumu yake ya Februali 2010 na kwa mujibu wa kanuni hiyo inatoa mamlaka kwa mahakama hiyo kufanya mapitio ya hukumu yake.
Wakili Marando alieleza kuwa ombi lake amelileta chini ya kifungu cha 3 aya A ya Kanuni ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 , ikisomwa pamoja na Ibara 13 (3) (6)(a) ya Katiba ya nchi, litaja moja ya utelezi wa wazi wazi wa kisheria uliofanywa na mahakama hiyo, ni kwamba katika hukumu hiyo kuna baadhi ya aya inasomeka kuwa majaji hao walikubaliana na hoja yake iliyodai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakati inasikiliza kesi hiyo, ilikosoea kufuata utaratibu wa kurekodi ushahidi wa watoto waliokuja kutoa ushahidi katika kesi hiyo na kwamba mahakama ya rufaa ikasema licha ya taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto kukiukwa, mahakama yake iliona kuna ushahidi unaounga mkono na kwamba mahakama ya rufaa ilitumia ushahidi wa kuunga mkono ndiyo walioutumia kuwatia hatiani waomba rufaa kwa adhabu ya kifungo cha maisha.
“Waheshimiwa majaji kwasababu jopo lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi kuwa mahakama ya kisutu ilikosoea kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo ambao walidai walitendewa vibaya na waomba rufaa(Nguza na Papii), na sheria za nchi zipo wazi kabisa zina sema endapo mahakama itabaini kuwa mahakama ya chini ilikiuka taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo, basi ushahidi ule wa watoto wa dogo uliotumika katika mahakama ya chini kuwatia hatiani washitakiwa, ushahidi huo wa watoto unafutwa na waomba rufaa au washitakiwa wanaachiriwa na pia maamuzi ya kesi mbalimbali yaliyokwisha kutolewa na mahakama hii;
“Nafahamu ni kazi ngumu sana kuwashawishi nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februali 2010 ambapo mliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa uterezi huo wa kisheria niliouanisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na hoja yangu kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi watoto wadogo ,naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria inayosema wazi wazi kuwa endapo utaratibu wa kurekodi ushahidi wa mtoto utakiukwa basi ushahidi huo utafutwa na wateja wangu wataachiliwa huru, basi leo naiomba mahakama hii iwaachirie huru wateja wangu’ alidai Marando.
Kwa upande wao mawakili wa upande wa mjibu maombi (DPP),Angaza Mwipopo,Jackson Mlati, Imaculata Banzi na Joseph Pande waliomba mahakama hiyo itupilie mbali ombi hilo kwasababu sababu zote alizozitoa jana ni sababu ambazo alizitoa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamliwa katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februali mwaka 2010.
Jackson alidai kama Marando anaona hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari , basi angeomba mahakama hiyo impangie jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na siyo ombi lake kuja kusikilizwa na jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu ile ambayo Marando anadai ina dosari.
“Hoja za Marando ni za kirufaa, na hoja zake zote anazotaka kuonyesha hukumu ya mahakama hii ina dosari zilishaamriwa na mahakama hii wakati ikisiliza rufaa ya wateja wake mwaka 2010 na tunamtaka Marando aelewe kuwa hakuna maamuzi yasiyonamwisho hivyo sisi tunaomba ombi la Marando linalotaka mahakama hii ifanyiwe mapitio hukumu yake halina msingi”alidai wakili Jackson.
Aidha Jaji Kimaro alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili akaamuru waomba rufaa warejeshwe gerezani na kwamba mahakama itatoa tarehe ya kutoa uamuzi wake kuhusu maombi hayo kwa pande zote mbili.
Aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Addy Lyamuya, aliyekuwa jaji wa Mahakama Kuu Thomas Mihayo na jopo hilo la majaji wa tatu linaloundwa na Jaji Kimaro ,Massati na Mbarouk liliwatia hatiani kwa makosa ya kuwabaka watoto wadogo na likawahukumu kifungo cha maisha gerezani na hadi sasa wameishakaa gerezani kwa miaka kumi.
Mahakama ya Rufaa, Februali mwaka 2010 ,ilirekebisha hukumu ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Kisutu ambapo iliwaachiria huru waomba rufaa wawili katika kesi hiyo ambao ni watoto wa Nguza Vicking, Nguza Mbangu na Francis Nguza waliachiwa huru, huku Viking na Papi Kocha wakiendelea kutumikia kifungo chao hadi sasa.
Hata hivyo jana mahakama hiyo ilifurika wanamuziki, mashabiki, ndugu wa washitakiwa na wengine walilazimika kukaa sakafuni ambao walikuja kusikiliza kesi hiyo.
Na HPPINESS KATABAZI, Tanzania Daima
Taarifa mbili zimepachikwa hapo chini kwa uchambuzi wako, kutoka magazeti ya UHURU na TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment