TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
 “PRESS RELEASE” TAREHE  21.05.2014.
- JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI KATIKA MATUKIO TOFAUTI.
 
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUKUTWA NA POMBE KALI
 
- WAHAMIAJI HARAMU 17 WAKAMATWA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
 
KATIKA MISAKO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA 
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA  KUTOKANA NA MISAKO MBALIMBALI ILIYOFANYIKA. 
 KATIKA TUKIO HILO   JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA OSCAR S/O 
MBELEWA,[36],MKAZI WA KAFUNDO- IPINDA MKAZI WA KIJIJI CHA MAZIMBO  KWA 
KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI KG 72 KWENYE GUNIA AKIWA NA PIKIPIKI YAKE 
YENYE NO T.477 CMZ AINA YA  SANLG.   TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 
20.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI STAMICO, KIJIJI 
NA KATA YA MKOLA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. 
TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
AIDHA; JESHI LA POLISI MKOA
 WA MBEYA LINAMSHIKILIA CASIAN S/O JOSEPH, [19], MKAZI WA UBARUKU AKIWA 
NA BHANGI KETE 65, SAWA NA UZITO WA GRAM 325. TUKIO HILO LIMETOKEA 
TAREHE 20.05.2014 MAJIRA YA SAA 17:00HRS KATIKA KIJIJI NA KATA YA 
UBARUKU, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA
 KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
VILEVILE; JESHI LA 
POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA HASSAN S/O ISMAIL, [30], MKAZI WA 
MBUGANI  AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA YA  BOSS
 KATONI MOJA [01]. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 20.05.2014 MAJIRA YA SAA 
11:25HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUKUYU, KATA YA MWAYA, TARAFA YA 
NTEMBELA, WILAYA YA  KYELA,   MKOA WA MBEYA, TARATIBU ZA KISHERIA 
ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA 
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA WITO KWA
 JAMII KUACHA KUTUMIA BHANGI/POMBE HARAMUZILIZOPIGWA MARUFUKU KWANI NI 
KINYUME CHA SHERIA  NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA 
LINAWASHIKILIA NYABEDA S/O SAMSON, [32] RAIA NA MKAZI WA NCHINI BURUNDI 
PAMOJA NA WENZAKE 16 WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. AIDHA 
ALIKAMATWA MTANZANIA HAMIS S/O MWAKALINGA [29] MKAZI WA SOWETO AKIWA 
ANAWASAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU HAO. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 
20.05.2014 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO MWANJELWA STENDI YA TUKUYU, KATA 
YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA, TARATIBU ZA KISHERIA 
ZINAFANYWA ILI KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI. PAMOJA NA 
KUMFISHA MAHAKAMANI MTUHUMIWA HAMISA MWAKALINGA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA 
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA WITO KWA
 JAMII PINDI WANAPOWAONA/KUWATILIA MASHAKA WATU WASIOWAHAMU KUTOA 
TAARIFA KWENYE VYOMBO HUSIKA ILI WAKAMATWE NA KUHOJIWA.
Signed by:
 [ AHMED Z. MSANGI – SACP ].












0 comments:
Post a Comment