Sunday, 10 November 2013

WAZIRI ALIYE FUTWA KAZI MALAWI AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUJARIBU KUAA

Jana, polisi wa nchini Malawi walimtia mbaroni waziri wa zamani wa sheria wa nchi hiyo, Ralph Kasambara anayetuhumiwa kujaribu kumuua kwa kumpiga risasi afisa wa bajeti wa nchi hiyo aliyefichua kashfa ya ubadhirifu wya fedha za serikali.

Fahad Assani Waziri mpya wa Sheria wa Malawi amesema kuwa Kasambara alikamatwa na polisi asubuhi.

Msemaji wa Polisi, Kevin Maigwa amenukuliwa akiiambia BBC kuwa tayari wameshakusanya uthibitisho unaoonesha kuwa
 Kasambara alihusika katika shambuilo hilo ambapo anatuhumiwa kuongoza jaribio hilo la kutaka kumuuwa Paul Mphwiyo mkurugenzi wa bajeti wa Malawi mwezi Septemba mwaka huu wakati alipokuwa akiendesha gari kuelekea nyumbani kwake huko mji mkuu Lilongwe, Malawi.

Mphwiyo alipigwa risasi mara tatu tarehe 13 Septemba 2013 lakini alinusurika kifo. Alisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu na sasa hali yake imetengemaa ingawaje hajarudi nyumbani nchini kwake, Malawi.

Mphwiyo alifichua kashfa ya ubadhirifu wa zaidi ya dola milioni 1,000 mali ya serikali, sakata ambayo linatajwa kuwahusisha maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa serikali ya Malawi ambao tayari wametiwa mbaroni.

Rais wa Malawi Joyce Banda amesema jaribio la kumuua Mphwiyo lililenga kunyamazisha mapambano dhidi ya rushwa iliyokidhiri.

Kasambara alifukuzwa kazi mwezi uliopita kutoka kwenye cheo cha Uwaziri wa Sheria alichoteuliwa na Rais Banda punde tu alipoingia madarakani baada ya kifo cha Rais Bingu wa Mutharika mwezi Aprili mwaka jana.

Nchi zinazotoa msaada za Magharibi kwa asilimia 40% ambazo zimezuia misaada yao kwa nchi ya Malawi tokea mwezi jana zikiongozwa na Norway, zimekuwa zikimsihi Rais Banda apambane na rushwa katika nchi hiyo. Mojawapo ya mikakati aliyoifanya Rais Banda aliponyakua madaraka ilikuwa ni pamoja na kushusha thamani ya fedha ya nchi hiyo, Kwach
a.

 chanzo wavutiblog

0 comments: