Thursday, 7 November 2013

AL-SHABABU YASEMA WENYE TV NI MAKAFIRI ;YAPIGA MARUFUKU BARAWE

Kwa kutumia vipaaza sauti vilivyofungwa kwenye magari al-Shabaab waliwapiga marufuku watu wa Barawe kutoangalia televisheni, wakisema zinaharibu kanuni zao za Uislamu, na kuwaagiza kupelekea televisheni zao na madishi ya satelaiti kwa maofisa wa al-Shabaab..

Wanamgambo hao walitangaza marufuku hayo tarehe 28 Oktoba na waliwapa wakaazi siku tano kuwasilisha vifaa hivyo 
kwenye ofisi ya manispaa ya Barawe, alisema Mursal Yarisow, mzee wa kimila mwenye umri wa miaka 54 huko Barawe.

Kwa hakika nilishangaa wakati niliposikia kuhusu agizo la kikatili ambalo lilituzuia kutoangalia televisheni wakati tukiwa nyumbani kwetu," aliiambia Sabahi. "Idhaa pekee ambayo mimi na familia yangu huangalia ni zile za Somalia, kama vile Universal TV, Horn Cable TV na Somali Channel TV, ili kwamba tuweze kupata taarifa kuhusu habari za kidunia." "Sina uhakika wa wapi al-Shabaab waliona au kuangalia stesheni hizi nyingine ambazo wanasaema zinaharibu dini," alisema.

Marufuku hayo ni kisingizio cha kuzuia watu kutopata taarifa kuhusu habari na masuala yanayotokea hivi sasa kupitia stesheni za televisheni huru za Somalia: "Mimi na [wazee] wengine kama mimi ni watu wazima ambao tunaelewa kitu ambacho wanaume hawa wanalenga kwa kupiga marufuku televisheni," alisema. "Wanataka watu wabakie kuwa wajinga kwa chuki walio nayo Wasomali na dunia dhidi ya al-Shabaab, na wanataka wakaazi wa Barawe kuwa watu ambao masikio na macho yao yamezibwa."

Marufuku hayo yamekuja wiki tu baada ya shambulio lililofanywa na Meli ya Marekani huko Barawe yakimlenga kamanda wa al-Shabaab Abdulkadir Mohamed Abdulkadir, ambaye alijulikana kwa jina jingine Ikrima, ambaye aliaminika kuishi katika nyumba ufukweni ya eneo hilo.

Al-Shabaab waliripotiwa kutekeleza marufuku ya televisheni yanayofanana na hayo katika mji wa Shabelle ya Chini wa Bulomarer mwezi uliopita: "Al-Shabaab wanajihusisha na uhalifu mkubwa katika dunia, ambao ni kuwaua watu pasipo sababu au kuwapa jina kuwa wao si Waislamu. Wanawafanya watu kama vile wanawabadilisha kuwa Waislamu," Yarisow alisema. "Ninasikitishwa sana kwamba wanakuja kwa watu ambao ni Waislamu na kuhoji juu ya imani yao katika Uislamu."

Wakazi wenye televisheni kushutumiwa kuwa makafiri
Mkazi wa Barawe Saida Ali, mama mwenye umri wa miaka 41 na watoto sita, alionyesha hasira kuhusu uzuiaji.

"Mimi ni mama katika nyumba yangu, sio al-Shabaab. Nilipokuwa nikinunua TV kutoka sokoni katika umri huu wa miaka 41, sikununua kwa ajili ya kutazama filamu za matukio au kitu chochote ambacho ni kibaya kwa imani yangu," aliiambia Sabahi na kuongeza, "kama walikuwa waaminifu, yote waliyohitaji kutueleza ni kuwaongoza watoto wetu dhidi ya idhaa ambazo zinatangaza filamu za matukio badala ya kutuambia leteni mali yetu kituoni." "Al-Shabaab hawakutusambazia chochote na wametuvunjia haki zetu za binadamu. Wametufanya sisi kama watu wasiostaarabika ambao hatuna uelewa wa dini ya Kiislamu, lakini ni dhahiri kwamba al-Shabaab ni watu ambao hawana uelewa wa dini hiyo, na hakuna wasiwasi kuhusu hilo," alisema.

Liban Abdirahman, mwenye umri wa miaka 34, anayemiliki duka huko Barawe ambalo huuza taa na vifaa vingine, alisema alilalamikia uzuiaji wa al-Shabaab na kuchukua TV na dishi lake la satelaiti hadi katika ofisi za manispaa kama walivyoagiza: "Sisi ni raia na hatuna silaha hivyo tunalazimishwa kufuata mahitaji yoyote yasiyokuwa na sababu kutoka kwa al-Shabaab, kwa sababu yeyote ambaye hafuati amri na kushindwa kupeleka kituoni vifaa vya TV atashitakiwa kwa kuwa kafiri ambaye hafuati amri za Kiislamu," alisema.

Wanachokifanya al-Shabaab sio jambo jingine zaidi ya unyanyasaji, Abdirahman aliiambia Sabahi: "[Wao] wanavunja haki zetu kujua kinachotokea duniani na katika nchi yetu. Kimsingi hawapendi sisi kujua maendeleo ya wakaazi katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa al-Shabaab wanavyofanikiwa," alisema. "Hilo ni jambo kuu wanataka watu kuwa gizani."

Abdirahman alitoa wito kwa serikali ya Somalia kuingilia kati haraka na kumaliza unyanyasaji unaofanywa kwa watu wa Barawe na al-Shabaab: "Kuua watu sio jambo la ajabu kwa al-Shabaab," alisema Abdirahman. "Hawana mizizi wala ufuatiliaji wa Uislamu na kila mmoja anajua wanadanganya kuhusu Uislamu."

Wakazi walisema hawajui iwapo al-Shabaab wanakusudia kuharibu au kuuza seti za televisheni na vifaa vingine walivyovinyang'anya.


Chanzo cha taarifa:ni kwa hisani ya SABAHI

0 comments: