MWILI wa aliyekuwa msanii wa muziki wa
kizazi kipya, marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ sasa unatarajiwa kuwasili nchini
kesho badala ya leo kama ilivyotaarifiwa awali.M
Kwa
mujibu wa taarifa ya kamati ya mipango ya mazishi ya msanii huyo iliyotolewa
jana inayoongozwa na Kaka wa marehemu, Kenneth Mangwea, mwili huo utawasili
Jumapili majira ya saa 8, mchana na kisha kufuata taratibu zingine.
“Mwili
utafika nchini siku ya Jumapili majira ya saa nane mchana na sio Jumamosi
(leo), kama ilivyotaarifiwa hapo awali,” ilieleza taarifa hiyo.
Sababu
za mabadiliko hayo, imeelezwa ni kutokana na Watanzania waishio Afrika Kusini,
kuomba kutoa heshima za mwisho, Jumapili.
Kwa
hatua hiyo, kamati ilibainisha kuwa kwa wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya
jirani, watapata nafasi ya kuuaga mwili Jumatatu majira ya saa 2 asubuhi hadi 6
mchana na baada ya hapo, wataelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi, Jumanne.
Aidha,
kamati iliomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, huku ikiomba wadau
kuendelea kuwaombea kufanikisha salama shughuli hizo za mazishi
0 comments:
Post a Comment