Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za
makazi Mkuzo na kukaribishwa na wenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe (mwenye tisheti ya
pundamilia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika eneo la tukio ambako alizindua mradi huo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe
la msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na
Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani
Ruvuma jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Bw. David Misonge Shambwe na wa pili kushoto ni Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, kulia ni
Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais.
Rais
Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu (kulia),
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto)
na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata
utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Kaimu
Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw David Shambwe akitoa taarifa za
mradi wa huo wa gharama nafuu wa Mkuzo kwa Rais Dr. Jakaya Kikwete.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Cha Shirika la Nyumba la
Taifa (National Housing) Susan Omari akitoa maelezo kwa Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu mashine za kutengeneza matofali aina ya
Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ili
kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi vya vijana kuendelea na
mafunzo . Anayezishuhudia Mashine hizo ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna kajumulo Tibaijuka.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka
na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu wakizishuhudia mashine za
kufyatulia matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya
zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi
vya vijana kuendelea na mafunzo .
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza
katika hafla hiyo jana, kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe
Magufuli, wabunge na viongozi mbalimbali wa mkoa huo walioshuhudia
tukio hilo.
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, ambapo
aliziagiza halmashauri za miji kuzipa maeneo taasisi mbalimbali za umma
zinazojishughulisha na masuala ya uendelezaji miji ili waweze kupanga
miji vizuri na kuboresha madhari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na
mkewe mama Salma Kikwete wakiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Wananchi waliofika kushuhudia tukio la uzinduzi wakiwa wamejipanga kando ya barabara.
Msafara
wa Rais ukiondoka jana katika eneo la tukio baada ya kumaliza ufunguzi
wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
mojawapo ya nyumba iliyokuwa ya mfano wakati wa ufunguzi wa nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo
wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
Kikundi cha ngoma na burudani kikiburudisha hadhira iliyofika eneo hilo la Mkuzo kabla ya Rais kufika.
…………………………………………………………………………
Rais Kikwete amerejea kauli
yake aliyoitoa Kasera, Mkinga Tanga kwamba Halmashauri zizipatie taasisi
zingine zinazojishughulisha na uendelezaji miliki kama NSSF, PPF, GEPF,
PSPF, LAPF na kadhalika maeneo kwa masharti ili ziweze kujenga.
Rais Kikwete aliambiwa kuwa
katika eneo hilo la Mkuzo, shirika hilo limejenga kiasi cha nyumba 18 za
kuuza na zimejengwa kwa gharama ya sh. milioni 676.
Rais Kikwete pia ameambiwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge
Shambwe kuwa nyumba hizo zimejengwa katika kutekeleza kaulimbiu ya NHC
ya “Nyumba yangu, Maisha yangu” ambayo mpaka sasa inatekelezwa katika
mikoa 14. Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Januari mwaka jana na
unakamilika mwezi ujao, Agosti, 2014.
Nyumba hizo, ameambiwa Rais
Kikwete, kuwa zitauzwa kwa gharama ya kati ya sh. milioni 33 na 44 bila
kodi ya VAT lakini ambayo inaongezeka na kuwa kati ya milioni 44 na 52
kwa kutegemea ukubwa wa nyumba – kuanzia ya vyumba viwili hadi nyumba
vitatu. Rais Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani humo.
Mkuzo Housing
Estate ni mradi wa nyumba 18 zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji
ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo Zahanati , shule ya Chekechea
, maduka , sehemu za shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana
inayotoa fursa kwa watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vile vile
imezingatia nafasi za miundombinu kama vile mitaro na umeme.
Kila nyumba inajitegemea ikiwa
na eneo kubwa kwaajili ya matumizi binafsi ya wakazi pamoja na eneo la
maegesho ya magari hadi matatu.
Mkuzo Housing estate ina
nyumba za aina mbili, nyumba za vyumba vitatuna nyumba za vyumba viwili .
Nyumba za vyumba vitatu zin aukubwa wa mita za mraba 85 kwa zile zenye
jiko la nje na mita 70 zenye jiko la ndani. Huku nyumba ya vyumba viwili
ikiwa na mita za mraba 56. Zinauzwa kati ya Sh 33 milioni bila VAT na
44 milioni.
0 comments:
Post a Comment