Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani
(UNHCR), Joyce Mends-Cole akizungumza na baadhi ya wadau waliohudhuria
katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Nelson Mandela kabla ya
kusoma ujumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki
Mooniliyofanyika leo duniani kote na hapa nchini imeadhimishwa katika
shule ya watoto wenye mahitaji maalum na kudhaminiwa na Vodacom.
Na Mwandishi wetu
Wafanyakazi
wa Ubalozi wa Afrika ya kusini nchini Tanzania, Kituo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa (UNIC) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo Julai 18, 2014 wameungana na taasisi
na wananchi kutoka sehemu mbalimbali duniani katika kuadhimisha siku ya
Kimataifa ya aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini
aliyejitolea maisha yake kupigania na kuondoa vitendo vya ubaguzi wa
rangi na unyanyasaji nchini humo, hayati Nelson Mandela.
Siku
ya Mandela ilitangazwa na Umoja wa Mataifa kuadhimishwa tarehe ya leo
kila mwaka na imekuwa ikiadhimishwa siku kama hii sehemu mbalimbali
duniani ambapo taasisi mbalimbali hushiriki kufanya kazi za kujitolea
kuhudumia jamii kwa muda wa dakika 67 kumuenzi kiongozi huyu aliyeleta
mapinduzi makubwa yenye historia ya kipekee duniani.
Katika
kuienzi siku hii ya leo,Ubalozi wa Afrika Kusini nchini ,Kituo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), wafanyakazi wa kampuni ya simu za
mkononi ya Vodacom wameshiriki katika shughuli za kuhudumia jamii
ambapo wamesafisha mazingira ya shule ya watoto wenye mahitaji maalum
ya Sinza jijini Dar es Salaam ambapo pia wamegawa zawadi mbalimbali kwa
watoto wanaosoma shuleni hapo.
Kaimu
balozi wa Afrika kusini nchini, Terry Govender alisema wanajivunia kuwa
na kiongozi hodari kama Nelson Mandela ambaye alijitolea nusu ya maisha
yake kupigana dhidi ya ubaguzi nchini Afrika Kusini na kuwaasa watu
kufwata nyayo zake kwani ni mfano wa kuigwa duniani.
Kaimu
balozi wa Afrika Kusini nchini, Bw. Terry Govender akitoa shukrani kwa
wadau waliojumuika pamoja na Ubalozi huo kwenye maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Nelson Mandela yaliyofanyika leo jijini Dar katika shule ya
Watoto Wenye Mahitaji Maalumu Sinza Mapambano.
“Kama
ilivyokuwa kwa Nelson Mandela, alitumia muda wake na nguvu zake
kuhamasisha amani na usawa na kupigania haki za wanyonge, Mandela pia
kupitia mfuko wa watoto aliouanzisha, aliamini kuwa watoto wote
wanapaswa kufurahia kwa kutokuwepo kwa njaa, unyonyaji, unyanyasaji na
kutokuwa na makazi, hivyo ndio maana sisi tunashiriki kwa kuirudishia
jamii kile tulichonacho na kufurahi pamoja na hawa watoto”, alisema.
Akiongea
juu ya kushiriki katika tukio hili muhimu, Meneja Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema kuwa kampuni inaona fahari kubwa
kushiriki na kutoa baadhi vifaa muhimu katika siku ya kiongozi
mashuhuri duniani mwenye historia ya pekee katika mapambano ya
kutokomeza vitendo vya kufifisha haki za binadamu.
“Vodacom
tunajivunia kushiriki katika shughuli za kijamii za kuadhimisha siku
maalum ya kiongozi shupavu wa Afrika,hayati Nelson Mandela, aliyejitolea
maisha yake yote kupambana na vitendo vya ubaguzi wa rangi nchini
Afrika na kuhakikisha vinatokomezwa kwa njia ya amani”alisema Nkurlu.
Mwalimu
Mkuu wa shule ya Watoto Wenye Mahitaji Maalumu Sinza Mapambano, Simon
Milobo akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa waliofika shuleni hapo
kutumia muda wao wa dakika 67 kufanya kazi za kijamii za kujitolea
katika shule hiyo, kama usafi wa mazingira yanayoizunguka shule, kupaka
rangi baadhi ya madarasa, kupika, michezo mbalimbali na watoto hao
kuonyesha vipaji mbalimbali walivyonavyo vikihusishwa na namna Nelson
Mandela alivyokuwa akiwathamini na kuwapenda watoto.
Alisema
mbali na kumuenzi hayati Mandela kwa kutokomeza vitendo vya
ubaguzi,Vodacom inatambua mchango mkubwa wa kiongozi huyo alivyokuwa
mstari wa mbele kuhudumia jamii na moja ya sera ya kampuni ya Vodacom ni
kushiriki katika kazi za kuhudumia jamii.
“Kwetu
Vodacom kushiriki katika shughuli za kijamii ni moja ya sera yetu hivyo
siku hii ni muhimu kwetu kama kampuni na wafanyakazi wake wote na siku
zote tutakuwa mstari wa mbele kushiriki na kusaidia katika shughuli za
jamii.Alisema.
Hayati
Nelson Mandela ambaye alifariki mwaka jana Desemba atakumbukwa daima
kwa ushupavu wake wa kutokemeza vitendo vya kibaguzi nchini Afrika ya
Kusini na baada ya kustaafu aliendelea kuisaidia changamoto mbalimbali
za kijamii kupitia taasisi ya Mandela Foundation.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar, Ramadhani Madabida akizungumza neno wakati wa maadhimisho hayo.
Afisa
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Gloria Mtui akigawa T-shirt za Vodacom
meza kuu kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (mwenye kofia ya
blue).
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (Kushoto)pamoja
na Afisa wa Ubalozi wa Afrika ya Kusini Nkhetheleni Mphohoni na Afisa
Mawasiliano wa Vodacom, Gloria Mtui wakigawa zawadi za tisheti na kofia
kwa wanafunzi na wa shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Sinza
jijini Dar es Salam wakati wa maadhimisho ya siku ya Mandela
iliyoandaliwa na Ubalozi wa Afrika ya kusini nchini na kufanyika leo
shuleni hapo.
Baadhi
ya wadau kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, Makampuni mbalimbali na
Taasisi walioshiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Mandela kwenye shule
ya Watoto wenye Mahitaji Maalum, Sinza Mapambano.
Baadhi ya wanafunzi wa wanaosoma katika shule yenye mahitaji maalum ya Sinza jijini Dar es Salam,wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Nelson Mandela iliyoandaliwa na Ubalozi wa Afrika ya Kusini nchini kwa ushirikiano na Vodacom Tanzania.
Afisa
Habari wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Stella
Vuzo, (kulia) akibadilishana mawazo na maofisa wa kampuni ya Vodacom,
Matina Nkurlu na Gloria Mtui, kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa Afrika ya
Kusini Nkhetheleni Mphohoni ,wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa
ya Nelson Mandela iliyofanyika leo duniani kote na hapa nchini
iliyoandaliwa na Ubalozi wa Afrika ya kusini nchini na kuadhimishwa
katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Sinza jijini Dar es
Salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Pichani
ni baadhi ya wadau wakiwapaka rangi Watoto wa shule msingi wenye
Mahitaji Maalum wa Shule Sinza Mapambano wakati wa maadhimisho hayo.
Mmoja
wa watoto anayesoma kwenye shule hiyo akitazama taswira mbalimbali
kwenye simu ya mmoja wa wadau waliojumuika kufurahi pamoja na watoto hao
kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela.
Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akishirikiana na
mmoja wa watoto wa shule hiyo kukata nyasi kwenye mazingira ya shule
hiyo.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani
(UNHCR), Joyce Mends-Cole akishiriki kufanya usafi na baadhi ya
wafanyakazi wa shirika hilo ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Mandela
inayoadhimishwa kila mwaka Julai 18 duniani kote.
Afisa
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Gloria Mtui akishikiana na wanafunzi
wanaosoma katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Sinza jijini
Dar es Salam,kusafisha mazingira ya shule hiyo wakati wa maadhimisho ya
siku ya kimataifa ya Mandela iliyoandaliwa na Ubalozi wa Afrika ya
kusini nchini kwa ushirikiano wa Vodacom.
Baadhi
ya vijana kutoka katika kikundi cha WAKALI JOGGER wakishiriki zoezi la
kusafisha mtaro ulio nje ya uzio wa shule ya Watoto wenye Mahitaji
Maalum Sinza Mapambano jijini Dar.
Mdau
Lauren Kiiza kutoka UNIC akishiriki kusafisha mtaro wa shule Watoto
wenye Mahitaji Maalum Sinza Mapambano wakati wa maadhimisho Siku Mandela
Duniani iliyoadhimishwa duniani kote leo.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
akipiga picha kwenye bango la maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Nelson
Mandela.
0 comments:
Post a Comment