Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jafari
Kasisiko (katikati) Katibu wa Mkoa CHADEMA, Msafiri Wamalwa (kushoto),
Katibu wa BAWATA Bi. Malunga Simba wakiwa wanatangaza uamuzi wao wa
kujitoa CHADEMA mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) Jafari Kasisiko ,
Katibu wa mkoa Msafiri Wamalwa na Katibu wa Baraza la wanawake, Bi.
Malunga Simba wa chama hicho Mkoa wa Kigoma wametangaza kujizulu
nafasi zao na uanachama wa chama hicho na kuachia nyadhifa zao kuanzia
2014 Julai 18
Akitangaza
uamuzi huo kwa niaba ya wenzake mbele ya waandishi wa habari mkoani
Kigoma, Mwenyekiti Jafari Kasisiko, amesema yeye na wenzake wamefikia
uamuzi huo baada ya kuona kuwa CHADEMA kimepoteza sifa ya kuwa chama cha
kidemokrasia na kuwa chama cha kibabe.
“Sifa
kubwa ambayo ilikuwa imetufanya tuendelee kubakia Chadema ni kwamba
kilikuwa bado kinaendelea na sifa ya kuwa ni chama cha kidemokrasia,
lakini baada ya kufikia hatua sasa kwamba kimeanza kuwa chama cha kibabe
zaidi na kuanza kukiuka misingi ya demokrasia, kwa kweli sina sababu na
wenzangu ya kuendelea kubaki katika chama hichi,”alisema.
Mzee
Kasisiko ambaye aliondoka CCM mnamo mwaka 1985 na kukaa nje ya siasa
kwa muda kabla ya kujiunga Chadema mwaka 1994, alitoa mfano unaoonesha
CHADEMA, kukiuka misingi ya demokrasia kuwa ni suala la aliyekuwa Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, ambaye alivuliwa wadhifa wake
kufuatia kutangaza nia ya kutaka kugombea moja ya nafasi za juu ndani ya
chama hicho.
“Mheshimiwa
Zitto, kosa lake pekee ni kwa sababu alionesha nia ya kutaka kugombea
uenyekiti wa Chadema. Lakini ukipitia katiba ya Chadema tangu ukurasa wa
kwanza mpaka wa mwisho, hupati mahala panaposema ni kosa mtu kutamani
kugombea nafasi yoyote katika chama.”
“Yeye
kuonekana kuwa alikuwa na nia ya kutaka kugombea, na kikubwa zaidi
tayari alikuwa na watu wanaoumuunga mkono, na mimi nikiwa mmoja wao,
basi hili lionekana ni dhambi kubwa sana.”
“Kwa
hiyo katika Chadema tulikuja kugundua kwamba kumbe uenyekiti sasa hivi,
ukiacha uenyekiti wa zama za Mtei, uenyekiti zama za Makani lakini
uenyekiti chini ya mheshimiwa Mbowe ni kitu nyeti ambacho hatakiwi mtu
mwingine kugusa.”
“Kwa
hiyo kitendo hichi kwetu sisi kilionesha wazi kuwa Chadema wamefikia
mahala sasa hawako tayari kufuata taratibu za kidemokrasia.”
Alisema
pamoja na kwamba na wamechukua muda mrefu kabla ya kutangaza uamuzi huo
walikuwa na sababu za msingi ambazo ziliwafanya wasitangaze, lakini
tangu siku Zitto Kabwe alipovuliwa nyadhifa zake walikuwa hawana imani
tena na chama kwa sababu hawawezi kuwa ndani ya chama ambacho ni mamlaka
ya watu Fulani.
Kwa
upande wake Msafiri Wamalwa alisema kwa ridhaa yake bila kushawishiwa
na mtu ameamua kuondoka Chadema na kwamba kabla ya uamuzi huo alikaa
chini na kutafakari, wakati Malunga Simba alisema ameamua kutoka Chadema
kwa sababu ni chama ambacho hakina faida na wananchi.
Baada
ya kujiuzulu uongozi na uanachama wa Chadema, Mzee Ramadhani Kasisiko
alisema anajiunga na chama kipya cha siasa cha Allience for Change and
Transparency, ACT, lakini wenzake hawakuzungumzia kama kuna chama
wanachohamia ingawa Msafiri Wamalwa alisema atatafuta chama makini.
0 comments:
Post a Comment