MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday, 30 November 2013

CHADEMA MAJANGA: MW/KITI WA CHADEMA MKOA WA LINDI AJIUZULU

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi, Ally Chitanda, ametangaza kujiondoa katika nafasi hiyo akieleza kuchoshwa na uamuzi wa kikanda na kikabila unaoendelea ndani ya chama hicho.
Mbali na Uenyekiti, Chitanda  pia alikuwa  Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa na Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu- Sekretarieti nafasi ambayo pia alitangaza kujiuzulu jana, lakini akaahidi kuendelea kuwa mwanchama mwaminifu wa Chadema.
Hata hivyo katika maelezo yake ya sababu za kujiuzulu alisema: “Sioni sababu ya kuendelea kuwa mwana Chadema, sioni sababu ya kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi.”
“Sioni sababu ya kuwa kiongozi kwa kuwa kipaumbele cha Chadema ni kukijenga chama Kaskazini, basi sisi wa Lindi tunawatakia kila la heri….”
Alisema amefikia hatua hiyo baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya Chama hicho, kuwavua nyadhifa Zitto na mwenzake Dk Kitila Mkumbo wiki iliyopita.
Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa kuhusu uamuzi huo wa Chitanda alisema kuwa hawezi kumzunguzia kwa kuwa ni mtu mdogo katika chama akitaka atafutwe msemaji wa Chadema Tumaini Makene aliyesema: “Mwambieni Chitanda atoe barua ya uteuzi wake.”
 
Na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Posted  Jumapili,Decemba1  2013

ALIYE BAKWA tFUTIWA MAASADA MOSHI

 
Moshi. Uongozi wa Kijiji cha Kiria, Kata ya Mamba Kusini wilayani Moshi, Kilimanjaro umeiomba Serikali na taasisi zinazojihusisha na ukatili wa kijinsia kumsaidia mtoto mwenye umri wa miaka 13 aliyebakwa na kulawitiwa na baba yake mzazi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Doroth Mtui alisema mtoto huyo kwa sasa amehifadhiwa kwenye nyumba ya msamaria mwema na anahitaji matunzo na kupelekwa shule, jambo ambalo serikali ya kijiji imeshindwa.
Mtui alisema mtoto aliyekuwa darasa la kwanza kabla ya kuachishwa shule, anahitaji kuishi sehemu tofauti na mazingira ya nyumbani ili kumnusuru na tatizo la kisaikolojia.
Mtui alisema mtoto huyo alipaswa kurudishwa hospitalini wiki mbili toka alipofanyiwa uchunguzi 0ktoba 9 mwaka huu, lakini mpaka sasa hajarudishwa kwa vile hakuna mwenye uwezo wa kumsaidia.
“Uchunguzi unaonyesha kuwa ameharibika vibaya sehemu za siri na ameota nyama kwa ndani. Alipewa dawa na anatakiwa kurudi tena kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Mtui
.Na Rehema Matowo, Mwananchi
Posted  Jumapili,Decemba1  2013  

KINANA AMKALIA KOONI MKURUGENZI WA MBOZI

10


Mbozi. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Dk Charles Mkambachepa juzi alionja joto la jiwe baada ya Katibu Mkuu wa CCM,  Abdulrahaman Kinana kumtaka arudishe haraka Sh209 milioni za Saccos ya Chama cha Walimu zilizochukuliwa na halmashauri hiyo katika mazingira ya kutatanisha kuanzia Mei mwaka huu.
Hali hiyo ilijitokeza juzi jioni wakati Kinana alipozungumza na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi hususan walimu.
Dk Mkambachepa alilazimika kutamka wazi kwamba atahakikisha anawalipa fedha zote ifikapo mwishoni mwa Januari mwaka ujao na kwamba juzi hiyo aliwalipa zaidi ya Sh32 milioni kupunguza deni hilo.
Awali Kinana alipokea taarifa ya malalamiko lukuki ya walimu yakiwamo ya madai ya zaidi ya Sh1 bilioni na pia halmashauri kuchukua Sh209 milioni za makato ya walimu kwa ajili ya kurudisha mikopo ya Saccos.
Walimu walidai halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi mstaafu Edson Chelewa ilichukua fedha hizo ikidai zinatumika katika masuala ya kumpokea Rais Jakaya Kikwete kwenye sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Mbeya.

Kutokana na kauli hiyo, Katibu Mkuu wa CCM alisema huo ni uzushi wa hali ya juu na kuitaka halmashauri hiyo kuacha mara moja tabia ya kuwaonea walimu kwa kusingizia viongozi mambo mabaya ya fitina.
“Kuanzia sasa CCM imeamua kuingia kati kufuatilia matatizo ya walimu yakiwamo madai yao na kwa kweli itahakikisha yanalipwa” alisema.

Awali akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Baraza la Kata, Kinana aliwasihi Watanzania kuendelea kuiamini Serikali ya CCM akisisitiza inalenga kuwatetea wanyonge na kuboresha maisha.

 Na Lauden Mwambona, Mwananchi
Posted  Jumapili,Decemba1  2013  

WAINGEREZA WA TINDIKALI WALIA NA SERIKALI


 

Dar es Salaam. Familia ya Waingereza, Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa miaka 18, waliomwagiwa tindikali huko Zanzibar, wameiomba Serikali ya Uingereza kuishinikiza Tanzania kuharakisha kuwawajibisha waliohusika na tukio hilo.

Waingereza hao ambao walikuwa walimu wa kujitolea katika shule ya St Monica, Tomondo, Zanzibar, walimwagiwa tindikali na watu wawili wasiojulikana wakati walipokuwa kwenye matembezi ya jioni katika eneo la Mji Mkongwe Agosti 7, mwaka huu.

Baada ya tukio hilo lililowajeruhi kiasi kikubwa katika maeneo ya kifua na mikononi, walipewa matibabu katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, kisha wakarudishwa kwao kwa matibabu zaidi.

Alipowatembea wasichana hao hospitalini, Rais Jakaya Kikwete alisema tukio hilo limetia aibu kwa mataifa ya nje na kuliamuru Jeshi la Polisi kuhakikisha linawakamata na kuwafungulia mashtaka wote waliohusika.
Taarifa iliyosambazwa kwenye mtandao wa habari wa Polisi wa Kimataifa (Interpol) Kanda ya Tanzania, inaeleza kuwa familia ya wasichana hao hairidhishwi na namna Serikali ya Tanzania inavyolishughulikia suala hilo kwa kuwa hadi sasa imeshindwa kuwatambua wahusika.
Mtandao huo umemnukuu baba yake Trup, Marc alipokuwa akizungumza na Redio 4 ya BBC, kuwa kuna wingu zito lililotanda kuhusu kesi hiyo, kwa kuwa hadi sasa Serikali ya Zanzibar imeshindwa kuonyesha picha za wahusika ili zitambuliwe na wasichana hao, ingawa imekwisha kuwahoji watu kadhaa.
“Picha haziwezi kutumwa katika muundo bora unaokubaliwa na Interpol au Mamlaka za Uingereza, kutokana na sababu hizo hakuna hata mmoja ameshaziona hizo picha,” alisema Marc.
Naye baba mlezi wa Gee, Doug Morris, alisema: “Kama Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Jumuiya ya Madola wako makini kusaidia watu hao kufikishwa mbele ya sheria kwa niaba ya raia wa Uingereza, tulitegemea wafanye kila linalowezekana, lakini hakuna dalili zozote zinazoonekana za kutaka kuharakisha jambo hili.”
Aliongeza:“Kama wanamaanisha wanachokisema na ni muhimu kwao kuwatafuta waliotekeleza kitendo hicho ili wawafikishe kwenye vyombo vya sheria, basi watusaidie kwa kila njia ambayo wanaweza.
“Kila mtu ameanza kufikiri kuwa wanatuchezea, kila wiki tunakatishwa tamaa. Huu ni uharibifu ambao hauwezi kupita tu bila mtu kuadhibiwa kwa manufaa ya wasichana wale au mtu mwingine yeyote.

“Aina gani ya ujumbe unaoletwa, kwamba unaweza kufanya jambo baya halafu usifanywe kitu chochote?”
Alisema kuwa wangependa suala hilo lifike mwisho haraka iwezekanavyo ili haki itendeke.
Chanzo  mwananchi  
Na Mwandishi Wetu

CHALENJI CUP: ZANZIBAR YA CHAPWA 3-1

WENYEJI KENYA WAICHAPA SOUTH SUDAN!
JUMAPILI: KILI STARS v SOMALIA
KILI_MABINGWAWENYEJI wa CHALENJI CUP, Kenya, leo wameifunga South Sudan Bao 3-1 na Ethiopia pia kuichapa Zanzibar Bao 3-1 katika Mechi za Pili za Kundi A zilizochezwa leo huko Nyayo Stadium, Nairobi.
Kwenye Mechi ya Zanzibar na Ethiopia, Bao za Wahabeshi zilifungwa na Fasika Asfan, Dakika ya 5, Salahadin Bargicho, kwa penalti ya Dakika ya 37, na Yonathan Kebede kuingiza Bao la 3 katika Dakika ya 83.
Bao la Zanzibar lilifungwa na Awadh Juma Issa katika Dakika ya 68.
Katika Mechi iliyofuatia, Wenyeji Kenya walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 16 kwa Penati ya Joackins Atudo lakini South Sudan ilisawazisha katika Dakika ya 26 kwa Bao la Richard Jistin.
Katika Dakika ya 29, Jacob Keli aliifungia Kenya Bao la Pili na katika Dakika ya 70, Atudo alikosa kufunga Penati ambayo Kipa wa South Sudan aliokoa lakini Kenya wakapata Bao lao la 3 alilofunga David Owino katika Dakika ya 78.
Jumapili zipo Mechi 2 za Kundi B katika ya Kilimanjaro Stars na Somalia na Zambia watacheza na Burundi, Mechi zote zikiwa huko Nairobi Uwanja wa Nyayo.
MAKUNDI:
Kundi A
KUNDI B
KUNDI C
-Kenya
-Ethiopia
-Zanzibar
-South Sudan

-Tanzania Bara
-Zambia
-Burundi
-Somalia
-Uganda
-Rwanda
-Sudan
-Eritrea
**FAHAMU: Timu mbili za Juu kila Kundi zitasonga Robo Fainali pamoja na Washindi wa Tatu wawili Bora.
RATIBA/MATOKEO:
TAREHE
NA
MECHI
KUNDI
UWANJA
SAA
Jumatano Novemba 27
1
Zanzibar 2 South Sudan 1
A
Nyayo
1400

2
Kenya 0 Ethiopia 0
A
Nyayo
1630
Alhamisi Novemba 28
3
Burundi 2 Somalia 0
B
Machakos
1400

4
Kili Stars 1 Zambia 1
B
Machakos
1600
Ijumaa Novemba 29
5
Sudan 3 Eritrea 0
C
Machakos
1400

6
Uganda 1 Rwanda 0
C
Machakos
1600
Jumamosi Novemba 30
7
Ethiopia 3 Zanzibar 1
A
Nyayo
1400

8
South Sudan 1 Kenya 3
A
Nyayo
1600
Jumapili Desemba 1
9
Somalia v Kili Stars
B
Nyayo
1400

10
Zambia v Burundi
B
Nyayo
1600
Jumatatu Desemba 2
11
Sudan v Rwanda
C
Machakos
1400

12
Eritrea v Uganda
C
Machakos
1600
Jumanne Desemba 3
13
South Sudan v Ethiopia
A
Machakos
1400

14
Kenya v Zanzibar
A
Machakos
1600
Jumatano Desemba 4
15
Kili Stars v Burundi
B
Nyayo
1400

16
Somalia v Zambia
B
Nyayo
1600
Alhamisi Desemba 5
17
Rwanda v Eritrea
C
Nyayo
1400

18
Uganda v Sudan
C
Nyayo
1600
Ijumaa Desemba 6

MAPUMZIKO





ROBO FAINALI



Jumamosi Desemba 7
19
C1 v B2

Mombasa
BADO

20
A1 v 3 BORA 1

Mombasa
BADO
Jumapili Desemba 8
21
B1 v 3 BORA 2

Mombasa
BADO

22
A2 v C2

Mombasa
BADO
Jumatatu Desemba 9

MAPUMZIKO



Jumanne Desemba 10

NUSU FAINALI




23
Mshindi 19 v Mshindi 20


BADO

24
Mshindi 21 v Mshindi 22


BADO
Desemba 11

MAPUMZIKO



Alhamisi Desemba 12
25
Mshindi wa Tatu


1400

26
FAINALI


1600

KOMBE LA SHIRIKISHO: TP MAZEMBE YASHINDA 2-1LAKINI BINGWA CS SFAXIEN!!

MBWANA SAMATTA APIGA BAO LA PILI!!
KLABU ya Tunisia CS Sfaxien leo imetwaa Taji lao la 3 la Kombe la Shirikisho huko LubumbashiMBWANA_SAMATTA_IN_TPlicha ya kuchapwa Bao 2-1 na TP Mazembe.

MAGOLI:
TP Mazembe 2
-Cheibane Traore Dakika ya 10
-Mbwana Ally Samata 23
Club Sportif Sfaxien 1
-Fakhreddine Ben Youssef Dakika ya 88

CS Sfaxien wametwaa Kombe baada ya kushinda Mechi ya kwanza Bao 2-0 iliyochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Mji wa Sfax Nchini Tunisia na hivyo kuvikwa Ubingwa kwa Jumla ya Mabao 3-2.
Sfaxien wameshatwaa Kombe hili Mwaka 2007 na 2008 na 2010 walikuwa Washindi wa Pili.
Kwa kutwaa Kombe hili, CS Sfaxien wamezawadiwa Dola 660,000 na Mwezi Februari watacheza na Al Ahly ya Egypt kuwania CAF Super Cup.

LIGI KUU ENGLAND: ARSENAL YAPIGA 3, YAENDLEA KUJIZATITI KILELENI MWA LIGI

BPL2013LOGO
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Novemba 30
Aston Villa 0 Sunderland 0
Cardiff 0 Arsenal 3
Everton 4 Stoke 0
Norwich 1 Crystal Palace 0
West Ham 3 Fulham 0
[Saa za Bongo]
20:30 Newcastle v West Brom

EVERTON 4 STOKE 0
Bao za Deulofeu, Coleman, Oviedo na Lukaku, leo zimewapeleka Everton juu na kukamata Nafasi ya 4 katika Msimamo wa Ligi Kuu England walipoibwaga Stoke City Bao 4-0 Uwanjani Goodison Park.
VIKOSI:
Everton: Howard, Coleman, Oviedo, Distin, Jagielka, Deulofeu, Pienaar, Barry, McCarthy, Osman, Lukaku
Stoke: Begovic; Cameron, Shawcross, Muniesa, Pieters; Walters, Whelan, Nzonzi, Adam, Assaidi; Crouch

ASTON VILLA 0 SUNDERLAND 0
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Bacuna, Vlaar, Clark, Luna, Delph, Westwood, El Ahmadi, Agbonlahor, Benteke, Weimann
Sunderland: Mannone, Bardsley, Dossena, Brown, O'Shea, Ki, Gardner, Larsson, Borini, Giaccherini, Fletcher

WEST HAM 3 FULHAM 0
Sasa, bila shaka, Meneja wa Fulham, Martin Jol, yuko hatarini kumwaga unga  baada ya Timu yake kuchapwa Bao 3-0 na West Ham walipocheza Ugenini Uwanja wa Upton Park.
Bao za West Ham zilifungwa na Diame, Carlton Cole na Joe Cole.
VIKOSI:
West Ham: Jaaskelainen, McCartney, Nolan, Tomkins, Jarvis, Maiga, Noble, Collins, Demel, Diame, Downing.
Fulham: Stekelenburg; Zverotic, Hughes, Amorebieta, Richardson; Duff, Sidwell, Parker, Kasami; Taarabt; Bent.

CARDIFF CITY 0 ARSENAL 3
Bao 2 za Aaron Ramsey na moja la Mathieu Flamini zimewapa Arsenal ushindi wa Bao 3-0 walipocheza Ugenini na Cardiff City.
Ushindi huu umewafanya Arsenal wazidi kupaa kileleni wakiwa Pointi 7 mbele.
VIKOSI:
Cardiff: Marshall, Taylor, Caulker, Turner, Whittingham, Medel, Campbell, Kim, Mutch, Cowie, Theophile-Catherine.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Wilshere, Ramsey, Ozil, Cazorla, Giroud

NORWICH 1 CRYSTAL 0
Bao la Dakika ya 30 la Gary Hooper, limewapa Norwich City ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Crystal Palace waliokuwa na Menja mpya Tony Pulis ambae leo ndio rasmi alikuwa akianza kazi.
Kipigo hichi kimewabakisha Palace mkiani na Norwich kupanda hadi Nafasi ya 14.
VIKOSI:
Norwich: Ruddy; Martin, R Bennett, Bassong, Olsson; Fer, Howson, Redmond, Hoolahan, Elmander, Hooper
Crystal Palace: Speroni, Ward, Gabbidon, Delaney, Moxey, Jedinak, Dikgacoi, Bannan, Puncheon, Chamakh, Jerome

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili Desemba 1
15:00 Tottenham v Man United
17:05 Hull v Liverpool
19:10 Chelsea v Southampton
19:10 Man City v Swansea

kwahisani ya soka inbongo 
Saturday, 30 November 2013 

:KUZAGAA KWA SILAHA NA ONGEZEKO LA MAUJI TANZANIA (AUDIO SOPHIA KESSY)

Picture
Sophia Kessy | Mubelwa Bandio
Si jambo geni tena hivi sasa nchini Tanzania kusikia fulani kashambuliwa au kauawa kwa risasi.

Silaha za moto hapa nchini hasa zile zinazomilikiwa kiholela zimekuwa zikimilikiwa na kila anayetaka... kama vocha za simu.

Hata mtu mwenye uwezo kidogo, na asiye na sababu ya kuwa na silaha anaweza kumiliki silaha nyumbani kwake .

Bastola kwa sasa zimekuwa kama bidhaa ya utashi na watu wanazimiliki kama wanavyomiliki simu za mkononi.


Ungana na Sophia Kessy (L, pichani) na Mubelwa Bandio (R) katika sehemu hii ya kwanza kuangalia tatizo hili linaloonekana kuzidi kuathiri na kutishia maisha ya Watanzania wengi.


Source:  www.wavuti.com  Kwa kusikiliza sauti bofya hapa

TAARIFA YA KUSIMAMISHWA UONGOZI KWA MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYANI MUNDULI

TAARIFA KWA UMMA

Kwa niaba ya baraza la uongozi la mkoa wa Arusha, napenda kuujulisha umma wote kwa ujumla kuwa mwenyekiti wa wilaya ya monduli Mchungaji Amani Silanga Mollel amekoma/amesimamishwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya monduli kuanzia tarehe 29 Novemba 2013 kufuatia tuhuma nzito za uvunjifu wa kanuni za maadili ya chama.

Hatua hii imefikiwa baada ya kuthibitika na yeyé mwenyewe kukiri mbele ya kikao cha kamati tendaji ya wilaya ya monduli kilichoketi tarehe 29 Novemba 2013 saa NNE asubuhi kuwa alitoa tamko batili akitumia wadhifa wa mwenyekiti wa wilaya bila ridhaa ya kamati tendaji na huku akidanganya kuwa ni tamko kwa niaba ya wilaya ya monduli.

Katika tamko lake ametoa tuhuma dhidi ya wajumbe wa kamati kuu na viongozi wakuu wa kitaifa kwa maamuzi halali ya kikao cha kamati kuu huku akijua kuwa anavunja kanuni za chama kwa mujibu wa katiba ya chama toleo la mwaka 2006 ya 
Kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya KUMI, ibara ya 10 (X) “Kiongozi asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizoelezwa kwenye kanuni za chama”.

Sambamba na hilo, Mchungaji Amani Silanga ametoa tuhuma za uzushi, uongo na upotoshaji na kutaka kuaminisha jamii kuwa chadema ina makundi ya CHADEMA Asili na CHADEMA Family kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa na wa hatari kwa ustawi na umoja wa chama na kinyume na kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya KUMI, ibara ya 10 (VII), “Kiongozi anatakiwa kuwa mkweli na muwazi wakati wote hususani katika vikao halali na aachane na vikundi vya majungu, wadanganyifu (Rumour Mongers). Ni mwiko kwa kiongozi kujihusisha na upotoshaji wa maamuzi wa vikao halali”. 

Kamati tendaji ya wilaya ilipomtaka aonyeshe CHADEMA asili ni kina nani na CHADEMA family ni kina nani alishindwa kutoa maelezo yoyote ya maana na kufikia hatua ya kutaka kuvuruga kikao kwa kuleta vijana wahuni wapatao 17 ndani ya kikao ambao wengi walijulikana kuwa sio WANACHADEMA. Katika utambulisho wake wa majigambo Mchungaji Amani SIlanga kwa kiburi na kejeli amejitambulisha na kukiri kuwa yeye yupo kambi ya Zito Kabwe na hakuna wa kumfanya kitu maana ni mjumbe wa baraza kuu la chama. Maneno yake yalidhihirisha kuwa Mchungaji Amani Silanga anashiriki mpango wa kuunda makundi yasiyo na tija ndani ya chama na hivyo kuwa kinyume na sura hiyo hiyo ya kumi ya kanuni za uendeshaji kazi za chama ibara ya 10 (IX), “Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au wanachama wake”.

AZIMIO LA BARAZA LA UONGOZI LA MKOA WA ARUSHA:

Baraza la uongozi la mkoa lililoketi tarehe 29 Novemba 2013, limepokea mapendekezo ya kamati tendaji ya wilaya na kuzingatia hofu kubwa iliyoainishwa na kamati tendaji kufuatia matendo mengi yanayotia shaka ya uadilifu na uwezo wa kiuongozi wa Mchungaji Amani Silanga na hivyo baraza la uongozi la mkoa limeridhia kuwa amevunja kanuni za maadili ya chama sura ya KUMI ibara ya (VII) hadi (XII) na hivyo kupelekea ukomo wa yeye kuwa Mwenyekiti wa wilaya kuanzia tarehe 29 Novemba 2013. Baraza la mkoa likiwa mamlaka ya nidhamu kwa mujibu wa katiba ibara ya 6.3.6 (a) (iv) limemjulisha tuhuma zake na hatua hii stahiki iliyochukuliwa. Kwa vile Mchungaji Amani Silanga alikiri kosa hili mbele ya kamati tendaji ya wilaya bila kulijutia au kuomba msamaha, baraza la mkoa limechukua hatua hii stahiki kwa maslahi ya chama na kuwa uchunguzi zaidi utafanyika ili kufikia maamuzi makubwa zaidi ya tuhuma nyingi kwa mujibu wa kanuni za hatua za kinidhamu.

Baraza la uongozi la mkoa wa Arusha, linatoa onyo kwa wote ambao wapo katika mtandao huu mchafu, ama watoke wenyewe mapema maana hawatavumiliwa kamwe. Baraza la uongozi wa mkoa liliona kuwa Mchungaji Silanga amepotoka na hivyo yeyé kuendelea kuwepo ndani ya chama wakati wa uchunguzi wa tuhuma hizi nzito dhidi yake ni hatari zaidi kwa ustawi wa chama na hivyo baraza likaridhia kwa kuzingatia tafsiri ya katiba ya chama ibara ya 6.3.4 (c) wa yeyé kukoma uongozi na hivyo akae nje kwa muda na waliopotoka wenzake.


Amani Golugwa
Katibu wa CHADEMA – Mkoa wa Arusha.
(Kwa niaba ya Baraza la Uongozi la Mkoa wa Arusha)

 

TAARIFA YA KUSAINIWA KWA ITIFAKI YA UMOJA WA FEDHA WA AFRIKA MASHARIKI

Picture
L-R ni Rais: Pierre Nkurunzinza (Burundi), Jakaya Mrisho Kikwete (Tanzania), Uhuru Kenyatta (Kenya), Yoweri Museveni (Uganda) na Paul Kagame (Rwanda) muda mfupi baada ya kutia saini itifaki ya Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki (picha: Freddy Maro/IKULU)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo kwa pamoja wametia  saini itifaki ya Umoja wa Fedha  wa Afrika Mashariki, (The East African Monetary Union) katika hoteli ya Speke, Munyonyo  mjini Kampala.

Marais waliotia saini itifaki kwa niaba ya wananchi wao ni Jakaya  Mrisho Kikwete wa Tanzania, Pierre Nkurunziza wa Burundi, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda .

Mara baada ya utiwaji wa saini, itifaki ya Umoja wa Fedha itapelekwa Kwenye mabunge ya nchi wanachama kwa ajili ya 
kuridhia ifikapo Mwezi Julai mwaka 2014.

Utiaji wa saini huu unaanzisha mchakato wa kuelekea kuwa na sarafu moja ifikapo mwaka 2024 kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kikao cha viongozi pia kilishuhudia Rais Kenyatta akichukua Uenyekiti wa Jumuiya kutoka kwa Rais Museveni na kuelezea matarajio yake ya Jumuiya kukua zaidi na kuzitaka nchi wanachama kuelimisha zaidi wananchi wa Afrika Mashariki kuhusu faida za Ushirikiano huu.

Itifaki ya Umoja wa Fedha ni ya tatu baada ya itifaki ya Umoja wa Ushuru wa Forodha na itifaki ya soko la pamoja na hatimaye kuelekea kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki.

Katika mkutano wa Leo, mbele ya viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwanafunzi Peter Robert kutoka shule ya sekondari Tushikamane, Morogoro amepokea cheti na zawadi ya fedha taslimu baada ya kuibuka mshindi wa shindano la kuandika Insha inayohusu EAC.

Mara baada ya kikao,,Rais Kikwete amerejea jijini Mwanza kuendeleza na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Simiyu ambapo kesho tarehe 1, ataendelea na ziara katika Wilaya ya Busega.

Mwisho.

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Kampala, Uganda
30 Nov 2013
 

TAARIFA YA CHADEMA:UFAFANUZI KUHUSU TAMKO LA NDUGU A.O. CHITANDA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU A.O. CHITANDA

Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu A.O. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;

Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, mjadala wake kwa upande wa chama umeshafungwa, huku taratibu za kikatiba za ndani ya chama zikiendelea.

Pili suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni 

Friday, 29 November 2013

KINANA AWASILI VWAWA WILAYANI MBOZI


1
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh Abbas Kandoro mara baada ya kuwasili katika ofisi za chama hicho mjini Vwawa Wilaya ya Mbozi asubuhi hii akitokea wilaya ya Momba katika ziara yake ya kikazi ya mikoa mitatu Ruvuma, Mbeya na Njombe, Kinana ameongozana na ujumbe wake akiwa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBOZI 2Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro mara baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ku wasili mjini Vwawa wilayani Mbozi asubuhi hii, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi 3Baadhi ya wana CCM wakishiriki kucheza ngoma na kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.(P.T)
5
Baadhi ya machifu wa Mbozi wakisubiri kusalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
6Baadhi ya viongozi mbalimbali na wananchi wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili wilayani Mbozi. 8Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na mbunge wa jimbo la Mbozi mashariki Ndugu Godfrey Zambi akisalimiana na wana CCM wakati wa mapokezi hayo 9 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na machifu 10Wana CCM wakiwa katika mapokezi hayo 11
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifutrahia ngoma ya asili ya wanyiha iliyokuwa ikitumbuizwa katika mapokezi hayo.

MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA TCRA KANDA YA MBEYA YAFUNGULIWA

 
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Crispin Meela  ambaye amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Mbeya katika sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya TCRA Mkoani Mbeya akifungua sherehe hizo katika ukumbi wa Mtenda Soweto Jijini Mbeya.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Mbeya Mhandisi Deogratius Moyo akizungumza machache kuhusiana na maadhimisho ya sherehe za miaka 10 ya TCRA Mkoan wa Mbeya.


 


 
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Mbeya Mhandisi Deogratius Moyo akitoa mada katika maadhimisho haya

 

Wanahabari na wadau hawakuwa mbali katika kilele hicho
Mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa sherehe hizo.
Kwahisani yaNa Mbeya yetublog

KERO YA VIFUSI BARABARA YA VINGUNGUTI JIJI DAR ES SALAM


 Kifusi kilichowekwa na Kampuni ya ujenzi ya Patty Interplan ya jijini Dar es Salaam inayojenga barabara ya Vingunguti hadi Barakuda kimelalamikiwa na baadhi ya watumiaji wa barabara hiyo kuwa kimekuwa kereo kutokana na kutosambazwa kwa muda mrefu na kusababisha foleni.
Kibao cha Mkandarasi wa uwanja huo.