Sunday, 2 June 2013

VITA VYA SYRIA VYAZIDI KUTAPAKAA LIBNAN



Wapiganaji wa Libnan wanaosaidia serikali ya Syria wakiwa zamu kwenye mpaka na Syria
 Katika ishara nyengine kuonesha jinsi vita vya Syria vinavoathiri taratibu utulivu katika nchi ya jirani ya Libnan, askari huko wanasema wapiganaji kadha wa Syria waliuwawa Jumamosi usiku katika mapambano na vikundi vya Hezbollah nchini Libnan karibu na mpaka wa Syria.

Inaarifiwa mapigano hayo yalitokea mashariki mwa bonde la Bekaa katika mji wa Baalbek.
Jumamosi makombora na mizinga kadha ilirushwa dhidi ya eneo hilo na makombora zaidi yamepiga piya mitaa ya kusini mwa Beirut.
Wapiganaji wa Syria wamesema watafanya mashambulio ndani ya Libnan kulipiza wapiganaji wa Hezbollah kumsaidia kivita rais wa Syria, Bashar al Assad.

Chanzo bbc

0 comments: