Wanabalozi katika Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa wanasema kuwa Urusi imezinga mswada wa
azimio la kueleza wasiwasi kuhusu hali, hasa ya raia, kwenye mji wa
Syria wa Qusair ambao umezingirwa.
Mashambulio ya serikali dhidi ya mji
huo unaodhibitiwa na wapiganaji yameendelea kwa zaidi ya majuma mawili
na wakaazi wamenasa bila ya chakula, maji wala madawa.
Lakini wanabalozi wanasema Urusi haitaunga mkono
mswada huo wa azimio kwa sababu Umoja wa Mataifa haukushughulika wakati
mji huo ulipotekwa na wapiganaji.
Hapo jana Umoja wa Mataifa na Shirika la
Kimataifa la Msalaba Mwekundu, ICRC, yalitoa maombi kuwa wasaidizi
waruhusiwe kuingia Qusair.
Msemaji wa ICRC, Dibeh Fakhir, aliiambia BBC taarifa wanazopata kuhusu hali katika mji huo:
" Ripoti tunazopata zinasema kuna upungufu mkubwa wa maji, chakula na madawa.
Piya zinaeleza kuwa mamia ya raia wamejeruhiwa na hawawezi kupata matibabu.
Maelfu tayari wameshakimbia Qusair na maelfu
wanasaidiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Syria, likisaidiwa na ICRC
na mashirika mengine.
Hata hivo inaripotiwa maelfu bado wako ndani ya mji - kati yao ni mamia waliojeruhiwa vibaya lakini haiwezekani kuwatibu"
Alisema kuweza kusaidia inavyotakiwa, ICRC inahitaji kuwepo Qusair bila ya kuingiliwa kati na serikali.
Chanzo bbcswahili
0 comments:
Post a Comment