JESHI la Polisi mkoani Rukwa
linamshikilia Mwalimu Ased Job (31) kwa kumtorosha
mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 17 kisha kuishi naye
kinyumba kwa zaidi ya miezi miwili sasa.
Mwalimu
huyo ambaye anafanya kazi katika Idara ya
Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga anatuhumiwa
kuishi na mwanafunzi huyo anayesoma kidato
cha pili kama mkewe kwa kipindi hicho chote.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Peter Ngusa, akithibitisha kutokea kwa
tukio hilo alisema lilitokea Februari mwaka huu baada
ya mtuhumiwa kumtorosha mwanafunzi huyo na kumpeleka
mkoani Mbeya kisha kufanya taratibu za uhamisho kwa lengo la kumhamishia mkoani
Mbeya ili akaishi naye huko.
“Baada
ya kukamilisha uhamisho huo mwanafunzi huyo alihamia mkoani
Mbeya kisha akaanza kuishi na mwalimu huyo
kinyumba hadi mwisho mwa Mei mwaka huu
alipomrejesha mjini Sumbawanga na kuendelea
kuishi naye kinyumba kisha baadaye kukamatwa,” alisema.
Kwa
mujibu wa Ngusa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo
kunatokana na taarifa za siri za wasamaria wema na
kwamba anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote
mara baada ya ya upelelezi wa awali dhidi ya
shauri lake kukamilika.
CHANZO: TANZNAIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment