Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema angalau akipata siku 10 za maandalizi kwa ajili ya kikosi chake anaweza kufanya vema dhidi ya Algeria.
Stars itaivaa Algeria Novemba, mwaka huu katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.
Stars imepata nafasi hiyo baada ya kuitoa Malawi kwa jumla ya mabao 2-1 katika mechi mbili za jijini Dar es Salaam na baadaye Blantyre.
Mkwasa ameiambia SLAEHJEMBE kwamba anajaribu kufanya jitihada angalau siku 10 zipatikane kwa ajili ya maandalizi.
“Siku kumi angalau zinaweza kutupa picha. Kwa kawaida hadi sasa kuna simu tatu za maandalizi ambazo naamini hazitoshi.
“Kama simu hizo kumi zitapatikana, nitafurahi sana kwa kuwa itakuwa ni msaada kwa maana ya maandalizi,” alisema Mkwasa.
Kabla ya kuivaa Nigeria kuwania kucheza Afcon na baadaye Malawi kuwania kucheza Kombe la Dunia. Stars iliweka kambi kwenye mji wa Kartepe nchini Uturuki na matunda yakaonekana.












0 comments:
Post a Comment