Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao
MGOGORO
ulio likumba kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi (Mbeya) baina ya
waumini walioungana na baadhi ya wachungaji dhidi ya Askofu wa jimbo hilo
Alikisa Cheyo umemaliza baada ya kufishana mbele ya kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Wilaya.
Hatua
hiyo ilifikiwa Julai 16 mwaka huu baada ya mgogoro huo kudumu kwa zaidi ya
mwaka mmoja baina ya pande hizo mbili zilizotofautiana ndani ya kanisa hilo,
kufikishwa mbele ya kamati ya ulinzi na usalama, chini ya Mwenyekiti wake, Mkuu
wa Wilaya, Dk. Norman Sigalla.
Mgororo
huo umefikia katika hatua hiyo ikiwa ni siku tano tangu baadhi ya
wachungaji na waumini wa kanisa hilo ambao walikuwa na makufuri, na
Minyororo kuvamia na kisha kuteka na kufunga,lango kuu pamoja na milango
yote ya ofisi wakishinikiza kujiuzuru
kwa Askofu huyo
Taarifa
za kuaminika kutoka ndani ya kikaoo hicho kilicho fanyika katika ofisi za Mkuu
wa Wilaya na kudumu kwa zaidi ya saa tatu,pande zote mbili zinazo tofautiana
zilikiri wazi kwamba zilikiuka taratibu za kanisa na kuvunja
katiba.
Akizungumza
na Mbeya yetu moja wawajumbe walioshiriki kikao hicho na kuomba jina lake
liifadhiwa alisema kuwa kikao hicho kilikuwa na zaidi ya 30 na muafaka
ulifikiwa baada ya Askofu Cheyo kuonesha hekima na busara kubwa ambapo
alionyesha dhairi alikuwa na dhamira ya kweli ya kuliokoa kanisa hilo katika
migogoro na kwamba hekima hiyo ingeonyeshwa tangu awali wasingelifika hapo
walipofikia.
Akifafanua
zaidi, mpaka Askofu huyo kufikia hatua kutoa maneno ya hekima ni baada ya Mkuu
wa Wilaya, Dk. Sigalla kuonesha jinsi serikali ilivyochukizwa na mgogoro huo,
ambao ulionekana kuvuka mipaka na kuashiria uvunjifu wa amani katika Wilaya
yake na Mkoa kwa ujumla.
“Ni
seme wazi maneno ya Mkuu wa Wilaya kwamba serikali haiwezi kulinda fikra
za waumini waliochukia, ingawa itaweza kupeleka askari, lakini haiwezi kulinda
mipango ya kuchoma makanisa yalimgusa sana Askofu Cheyo wetu na mungu
akamuongoza na kuonesha busara na hekima juu ya suala hilo” alisema Mjumbe huyo
Taarifa
zinaeleza kuwa Askofu Cheyo, ambaye ni baba wa kiroho ndani ya kanisa
hilo, alipopewa nafasi ya kueleza hali ya mgogoro huo na nini kifanyike,
alisema kimsingi, Mwenyekiti aliyesimamishwa Nosigwe Buya alifanya makosa ya
kiutendaji pekee.
Hivyo,
ili aweze kusamehewa na kurudishwa katika nafasi yake , anapaswa kuomba radhi
kwa makosa yake ya kiutendaji na ndipo Halmashauri Kuu iweze kumfikiria na
hatimaye kumrudisha kwenye nafasi yake.
Taarifa
zaidi toka ndani ya kikao hicho, zinadai kuwa Baada ya maneno hayo ya Askofu,
ndipo Mwenyekiti aliyesimamishwa Buya alisema kimsingi hana tatizo, lakini
haamini kama kauli hiyo ya askofu ina ukweli.
“Sina
uhakika na Askofu kwa kuwa amekuwa na tabia ya kubadilika badilika na kushindwa
kusimama kwenye kauli zake mara nyingi, hivyo kama atakihakikishia ukweli kikao
hiki, basi mimi sita kuwa na mengi zaidi ila isipokuwa lazima nimiweke
masharti” chanzo hicho kilimnukuu Mwenyekiti Buya.
Mara
baada ya kauli hiyo Buya alidaiwa kutoa masharti mawili, ambayo ni
kutaka Makamu Mwenyekiti Zacharia Sichone,ambaye ndiye mtendaji Mkuu wa
shughuli zote za kanisa na Halmashauri kuu kusambaza taarifa ya tume
iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ubadhirifu fedha zaidi ya shiloindi milioni
200/ itolewa na kusambazwa katika shirika zote 213 na idara zote za kanisa
hilo.
Wakati
sharti la pili lililo tolewa na Mwenyekiti huyo aliye simamishwa ni kama
taarifa hiyo ya ubadhirifu itaoneka si za kweli basi aombwe radhi ili kosa la
kiutendaji lidhihirike, baada ya vinara hao kutoa masharti hayo,
yalionekana kuungwa mkono na wajumbe wote, na huyo ukawa ndo mwisho na
muafaka wa mgogoro huo.
Mjumbe
huyo alibainisha kuwa mbali na Busara za Askofu na Mkuu wa Wilaya,alisema
shukurani za pekee ni Mchungaji Hakimu Mwandenuka kutoka Usharika wa
Tunduma ambaye ni mmoja wa wajumbe pale Mungu aliupo Muongoza kutumia vifungu
vya kutoka biblia takatifu katika kitabu cha Waebrania sura ya 12 , aya
ya 14 hadi 15, maneno yaliyo wagusa karibia wajumbe wote.
“Una
jua maneno aliyo yasoma Mchungaji Mwandemula yaliwagusa sana wajumbe nayo
yanasomeka ‘Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo ndio
utakatifu ambao hapana mtu atakayemuona bwana, asipokuwa nao, kwani shina la
uchungu lisije chipuka na kuwasumbua na watu wengi watatiwa unajisi kwa hilo
”.alisema Mjumbe huyo
Kanisa
hilo liliingia katika mgogoro huku wachungaji 20 na baadhi ya waumini,
wakiwemo wazee wa mabaraza ya kanisa hilo, wakipinga uamuzi uliofanywa na
Halmashauri kuu yaJimbo hilo huku Askofu Cheyo akitajwa kuwa kinara katika
uamuzi wa kumuondoa katika nafasi yake aliyekuwa Mwenyekiti Buya hatua iliyo
pelekea baadhi ya sharika kususa kupeleka sadaka ofisi kuu ya jimbo.
Mwisho
Na Mwandishi wetu
|
0 comments:
Post a Comment