Monday, 14 July 2014

MABINGWA MAN CITY WAANZA KWA KICHAPO, WAPYA FERNANDO, CABALLERO NDANI!

MABINGWA wa England Manchester City wameanza matayarisho yao kwa ajili ya Msimu mpya kwa kuchapwa Bao 2-0 na Dundee huko Dens Park, Jijini Dundee, Scotland.
FERNANDO-MAN-CITYMan City walichezesha Kikosi cha nguvu ambacho kilikuwa na Wachezaji wao wapya, Kipa Willy Caballero na Kiungo Fernando.
Caballero amehamia City kutoka Malaga ya Spain na Fernando ametoka FC Porto ya Ureno.
Mbali yao hao, City pia ilikuwa na Wachezaji wao wa kawaida kina Jesus Navas, Stevan Jovetic, Kolarov na Nasri.
Lakini Kikosi cha City bado hakna Wachezaji wao walioshiriki Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil wakiwa na Nchi zao kwani bado wapo Likizo na wengine wakiendelea na Mashindano.
Gary Harkins ndie aliefunga Bao la Kwanza la Dundee Dakika ya 27 baada Kipa mpya Willy Caballero kuokoa Penati aliyopiga yeye mwenyewe na Mpira kumrudia na kufunga.
Bao la Pili lilifungwa Dakika ya 38 na Luka Tankulic baada kupokea Krosi ya Harkins na kupiga Mpira uliombabatiza Beki Dedryck Boyata na kutinga.
VIKOSI:
Dundee: Adam, Irvine, Mcpake, Trialist, Dyer, Mcbride, Thomson, Trialist, Harkins, Mcalister, Trialist
Subs: Letheren, Davidson, Riley, Macdonald, Roberts, Stewart, Benedictus
Goals: Harkins, Tankulic
Manchester City: Caballero, Bossaerts (Richards 46), Kolarov (Leigh 46), Denayer (Rekik 46), Boyata (Nastasic 46), Navas (Garcia 46), Fernando (Zuculini 46), Rodwell (Nasri 46), Huws, Jovetic (Negredo 46), Guidetti (Sinclair 46)
MAN CITY
MECHI ZA KUJIPIMA KABLA MSIMU KUANZA
13 Julai Dundee 2 Man City 0
18 Julai Heart of Midlothian (A), Tynecastle
23 Julai Sporting Kansas (A), Kansas, USA
Guinness International Champions Cup
27 Julai AC Milan (N), Heinz Field, USA
30 Julai Liverpool (N), New York, USA
2 Agosti Olympiacos (N), Bank Stadium, USA
4 Agosti [Kama watafika Fainali] Miami, USA
**(A)=Ugenini, N (N)=Ugenini kwa Timu zote mbili

0 comments: