Baadhi ya washiriki wa kongamano la Global Academy for Oil and Gas wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa kongamano hilo
Mtendaji
wa TMAA, Giley shumika akiwa na mratibu wa kongamano hilo kutoka nchini
uingereza wakielekea ndani ya ukumbi wa hotel ya Maount meru
Mahmoud Ahmad Arusha
Zaidi ya
washiriki 56 wanashiriki katika Kongamano la kujadili sekta ya uziduaji
na uchanjuaji wa sekta ya madini mafuta na gesi katika sekta za
sheria,kanuni,sera na mikataba kwa watendaji wa sekta hiyo kutoka kwenye
nchi za jumuiya ya Afrika mashariki.
Akizungumza na
vyombo vya habari mkuu wa kitengo cha madini kanda ya kaskazini(tmg)
Mhandisi Gilay Shamika alisema kuwa kongamano hilo la siku mbili
lilovuta wadau wa sekta ya madini kutoka nchi za Kenya Uganda na wenyeji
Tanzania na kuandaliwa na taasisi ya Global Academy ya nchini
Uingereza.
Shamika alisema
kuwa sekta ya madini na gesi imekuwa na changamoto mbali mbali ambazo
zinahitaji elimu na ufahamu wa hali ya juu kwenye Nyanja hiyo hivyo
wanakutana kujadiliana kwa pamoja na wenzao kuweza kupata uelewa zaidi.
Aidha alisema
kuwa wadau hao kutoka sekta za sheria,madini na fedha ndioyo wanahusika
katika kongamano hilo huku wakipata uelewa ni jinsi gani watakavyoweza
kuongeza kiwango cha uchangiaji wa pato la taifa kutokana sekta ya
madini hususani Mafuta na Gesi.
Giley alisema
kuwa sekta ya madini hususani kwenye eneo la Mafuta na gesi limekuwa na
changamoto mbali mbali hivyo ni sekta muhimu kuielewa kwa mapana hivyo
wao na taasisi hiyo wanajadili kuweza kuzinufaisha nchi za ukanda huu.













0 comments:
Post a Comment