Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Suleiman Nkamia
akizunguza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea msaada wa
Hundi yenye thamani ya Dolla za Kimarekani 93,000 kutoka kwa Kampuni ya
Bakhresa Group kwa ajili ya kusaidia timu za wanamichezo wanaoshiriki
mashindano ya Jumuiya ya Madola jijini Glasgow Scotland jijini Dar es
Salaam leo (jana), katikati ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Said Muhammad
Said Abeid na Meneja Chapa wa Kampuni hiyo Bw. Abubaker S.A.
Kulia
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Suleiman
Nkamia akipeana mkono na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa Group, Said
Muhammad Said Abeid mara baada ya kumkabithi Hundi yenye thamani ya Dola
za Kimarekani 93,000 kutoka kwa Kampuni ya Bakhresa Group kwa ajili ya
kusaidia timu za wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya
Madola jijini Glasgow Scotland. Makabidhiano hayo yamefanyika katika
Ukumbi wa Wizara ya Habari leo jijini Dar es Salaam .
Picha na Frank Shija
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini., WHVUM
Na Rose Masaka-MAELEZO.
NAIBU
WAZIRI wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Juma Nkamia
amemuomba mmiliki wa kiwanja cha michezo cha Azam Complex Bw. Said
Salim Bakhresa kutoa ruhusa kwa wachezaji wa Tanzania kufanya mazoezi
katika uwanja huo hasa wakati wa usiku ili ziweze kuwa katika nafasi
nzuri na zipate uzoefu wa kucheza muda huo.
Hayo
yamesemwa leo na Mhe. Nkamia katika kikao cha kukabidhiwa cheki na
Bw. Bakhresa yenye thamani ya Dola 93,000 ili kuisaidia timu ya Taifa
ya riadha kufika Glasgow, Scotland pamoja na mahitaji mengine kama jezi
na vifaa.
“Fedha
hii itasaidia timu yetu yenye wachezaji 39 ,makocha, pamoja na walimu
waliotoka China kuweza kurudi salama.” Alisema Nkamia.
Aidha,
Mhe. Nkamia ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuweza kuzungumza na
wachezaji hao na kuwakabidhi bendera ya Taifa huko waendako.
Bw.
Bakhresa amesema kuwa anaisapoti timu ya Taifa kwenda Scotland kwa
sababu michezo siyo mpira wa miguu tu na amefafanua kuwa mashindano ya
michezo ni kitu muhimu katika nchi na kinaleta maendeleo.
“Tunachokipata
kinatokana na jasho la watanzania na tunakirudisha kwa
watanzania,Tanzania inajengwa na watanzania wenyewe siyo watu wa nje”.
Alisema Bakhresa.















0 comments:
Post a Comment