Mimi na likizo tu! Robin van Persie amepewa wiki tatu za mapumziko baada ya kumalizika kwa kombe la dunia.
ROBIN van Persie amepewa likizo ya wiki tatu na kocha wa Manchester United, Louis van Gaal na hataungana na kikosi cha klabu hiyo kwa safari ya America.
Mshambuliaji huyo wa Uholanzi aliweka
wazi kuwa anahitaji likizo baada ya Wadachi kumaliza katika nafasi ya
tatu ya kombe la dunia nchini Brazil.
Hii ni tofauti kwa Wayne Rooney, kwani
yeye amelazimika kukatisha likizo na kuungana na timu katika maandalizi
ya kabla ya msimu.
Van Persie alikosa mechi 8 mwishoni mwa
msimu uliopita na alikuwa anakaribia kumaliza bila kufunga katika mechi
ya jumamosi usiku dhidi ya wenyeji Brazil.
Hatakuwepo Marekani: Kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal ameamua kumpa likizo nyota wake.
Mshambuliaji huyo alicheza dakika 548
katika mashindano yote na Van Gaal ameona anahitaji kupumzika ili kurudi
na nguvu mpya kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu soka nchini
England.
"Nahitaji likizo," alisema Van Persie.
"Yalikuwa mashindano magumu. Kila mechi nilicheza kadiri niwezavyo.
Ndivyo ilivyokuwa, haikuwa rahisi".
Wakati huo huo imekuwa tofauti kwa Rooney, mchezaji mwenzake na Van Persie .
Maamuzi hayo ya kwanza kwa Van Gaal akianza kazi Man United, yanakuwa na utata ingawa yanaonekana kuwa sahihi.
Van Persie alikosa mechi 27 za Man United msimu uliopita, na hivyo ikipewa likizo anaweza kupata muda mzuri wa kukusanya nguvu.
Alionesha kiwango kizuri katika fainali
za kombe la dunia. Nyota huyo mwenye miaka 30 alifunga mabao manne
likiwemo la kichwa maridadi dhidi ya Hispania katika mchezo wa ufunguzi
na alikuwa mshambuliaji chaguo la kwanza la Van Gaal.
Pia Van Gaal amekuwa na uhusiano mzuri na Van Persie na anatarajia kumpa majukumu ya unahodha wa United badala ya Wayne Rooney.
Mwishoni mwa wiki, Van Gaal alimsifu
sana nyota wake ." Kama unajua alitoka wapi na amefanya nini, unachoweza
kufanya ni kumpongeza tu," alisema kocha huyu mwenye miaka 62.












0 comments:
Post a Comment