Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na ujumbe kutoka Chuo cha
St. Thomas cha Marekani uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo
Julai 16, 2014
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Y. Sefue leo tarehe 16 Julai, 2014 amekutana na wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Mt. Thomas cha Minnesota, Marekani wanaotembelea Tanzania
kujifunza uzoefu wa Tanzania katika masuala ya kiuongozi na anuwai ya
tamaduni. Wanafunzi hao ambao kwa idadi yao ni wanafunzi 14 wanaochukua
Shahada za Uzamivu na Uzamivu katika masuala ya Uongozi wa Kimataifa
pamoja na Wakufunzi wao wawili, Dkt. Jean Pierre Bongila na Dkt. Artika
Tyner.
Mkutano huu ni
mwendelezo wa mkutano kama huu ambao Katibu Mkuu Kiongozi aliufanya
mwaka jana na kundi jingine la wanafunzi kutoka Chuo hicho ambapo
aliwapa uzoefu wa uongozi na anuwai ya tamaduni katika Tanzania, Afrika
na katika medani za kimataifa.
Kwa kutambua umuhimu
wa nasaha walizozipata wanafunzi wa mwaka jana, Chuo hicho kiliomba na
kukubaliwa fursa nyingine ya kuonana na Katibu Mkuu Kiongozi. Ziara ya
wanafunzi hao ilianzia Arusha tangu tarehe 12 Julai, 2014 na itamalizika
tarehe 17 Julai, 2014.
Pamoja na kupata fursa
ya kuonana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha,
wanafunzi hao walipata pia muda wa kutembelea vivutio mbalimbali vya
utalii vilivyopo Arusha na baadaye Zanzibar. Na matarajio ni kuwa
wanafunzi hao watakuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania sehemu
mbalimbali za dunia watakakokwenda kufanya kazi.
Kwa ujumla, wanafunzi
wamepata fursa nzuri ya kuuliza maswali yaliyogusa maeneo yote
yanayohusu uongozi, siasa, uchumi, elimu, afya na utamaduni ambayo
yalipata ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.












0 comments:
Post a Comment