Timu
ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya Miaka 17, Serengeti Boys, Leo
hii imetoka Sare ya 0-0 na wenzao wa Afrika Kusini, Amajimbos, kwenye
Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Pili ya Mashindano ya Afrika, CAN U-15, ya
kusaka nafasi ya kucheza Fainali huko Niger Mwakani.
Mechi hii ya Leo ilichezwa huko Azam
Complex, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam na Timu hizi
zitarudiana huko Afrika Kusini Wikiendi ya kuanzia Agosti Mosi.
Mshindi kati ya Serengeti Boys na
Amajimbos atakutana na Mshindi kati ya Egypt na Congo katika Mechi ya
Raundi ya Mwisho ambayo itatoa Timu 7 kuungana na Wenyeji Niger kwenye
Fainali.
Fainali hizo zitachezwa kuanzia Februari
15 hadi Machi 1 Mwaka 2015 na Timu ambazo zitatinga Nusu Fainali ya
Mashindano hayo zitacheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa U-17
huko Chile Mwaka 2015.
VIKOSI:
Serengeti Boys:
Mitacha Mnacha, Abdala Jumanne, Issa Baky, Adolph Mutasingwa, Martin
Kiggi, Omar Wayne, Athanas Mdam, Ali Mabuyu, Abdul Bitebo, Prosper
Mushi, Baraka Yussuf
Amajimbos: Mondili
Mpoto, Nelson Maluleke, Simon Nqoi, Notha Ngcobo, Keanu Cupido, Tendo
Mukumela, Katlego Mohamme, Athenkosi Dlala, Sibongankonke Mbatha, Luvuyo
Mkatshana, Khanyiso Nayo
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Julai 18
Tanzania 0 South Africa 0
Jumamosi Julai 19
Uganda v Rwanda
Mozambique v Angola
Cameroon v Burkina Faso
Benin v Mali
Jumapili Julai 20
Zambia v Botswana
DR Congo v Nigeria
Togo v Senegal
Guinea v Morocco
Libya vs Cote d’Ivoire
Egypt v Congo
Ethiopia v Gabon
*South Sudan v Ghana
*Sierra Leone v Tunisia
*Zimejitoa [Ghana, Tunisia zatinga Raundi ya 3]
0 comments:
Post a Comment