
Boti la wakimbizi
Australia imedinda kutoa tamko
kuhusu ripoti kwamba imezuia maboti mawili yaliokuwa yakiwabeba
wakimbizi wa Tamil na badala yake ikaanza kuwakabidhi kwa wanamaji wa
Sri-lanka.
Serikali imesema kuwa haiwezi kuzungumza kuhusu
swala hilo kutokana na sababu za oparesheni zake,lakini mawaziri
wamesisitiza kuwa taifa hilo linachukua jukumu lake.Wana kampeni hatahivyo wanasema kuwa Australia linakiuka haki za kibinaadamu mbali na sheria za kimataifa.
Kuyazuia maboti ya wakimbizi kutofika nchini Australia ni miongoni mwa ahadi za kampeni zilizotolewa na waziri mkuu wa mrengo wa kulia Tony Abbot.












0 comments:
Post a Comment