Kwa hali hii ya wasisi na makada wa ccm kwenda ukawa ni wazi kwanba CCM uda wake wa kutawala uko ukingoni hivyo basi watanzania inabiti tujufunze kwamba kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho wake, ukifuatilia makada wengi sana wamefunja ukimya na kuona chama cha mapinduzi kwa sasa hakina jipya licha ya kwamba wao ndiyo wame kainzisha na kukikuza mpaka hapo kilipo,mtanzania funguka badilika
haya sasa nahuyu nae kaondoka nahuku Zikiwa zimebaki siku 5 kabla ya Oktoba 25, siku ambayo watanzania wataandika historia ya kuiweka madarakani serikali mpya ya awamu ya Tano, kada mwingine Mkongwe wa Chama hicho, ametangaza rasmi kujiweka kando.
Dkt. Eve Sinare, ambaye ni wakili wa kujitegemea aliyekuwa sehemu ya harakati za CCM, alitangaza jana kukihama chama hicho akidai kuwa kimepoteza sifa za utawala bora na kimeshindwa kuwahudumiwa wananchi kwa kuwapa elimu bora iliyotarajiwa.
Dkt. Eve Sinare aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA). Pia, ni Mwenyekiti Mtendaji wa Rex Attoneys na aliwahi kuteuliwa kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Bodi ya Huduma ya Dunia iliyoko Texas inayofahamika kwa jina la World Services Group (WSG).
Hata hivyo, kama alivyosema Balozi Juma Mwapachu wakati anahama chama hicho, Dkt. Eve Sinare ameeleza kuwa hatajiunga na chama chochote cha siasa.
0 comments:
Post a Comment