WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imewafukuza Mkuu wa Gereza la Kiteto mkoani Manyara na
Msaidizi wake, kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yao na kutumia mali za Serikali, kwenda kufanyia ujangili na kuiba nyara za Serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam JUMATANO Msemaji wa wizara hiyo, Isaac Nantanga, alisema maofisa hao ni pamoja na Mrakibu wa Magereza Ally Ramadhani Sauko na msaidizi wake ambaye ni Mratibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro.
Alisema maofisa hao walifukuzwa rasmi kazini Julai 29, mwaka huu na Katibu Mkuu wa wizara hiyo
kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha 34(6) cha Kanuni za Utumishi wa Magereza za mwaka 1997.
“Kufukuzwa kwao kunatokana na matumizi mabaya ya

madaraka kwa kuruhusu mali za Serikali, ilikiwemo gari na silaha kutumika katika kufanyia ujangili,” alisema Nantanga.
Maofisa hao Julai 23, mwaka huu wakiwa na wenzao wengine wawili ambao ni askari magereza wa gereza hilo la Kiteto Koplo Sylvester Dionice na Wada Barick, walikamatwa na kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Kati wakiwa na gari la jeshi la Magereza na silaha na kupakia nyara za Serikali huku dereva wa gari hiyo Sajenti Ketto Ramadhan akitoroka.
Baada ya uchunguzi wa awali, Jeshi la Magereza lilitoa taarifa ya kuwafukuza kazi askari hao watatu waliohusika kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza na watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi wa Polisi kukamilika.
Maofisa wawili ambao walikuwa wakuu wa gereza hilo, pamoja na kushtakiwa walivuliwa nafasi ya uongozi wao wakisubiri hatua zaidi za Wizara ambao nao sasa wamefukuzwa kazi na wanasubiri kesi yao mahakamani.

0 comments:
Post a Comment